MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Maji Yageuka Gesi, Lusano Aibua Ubunifu wa Nishati Safi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Makala > Maji Yageuka Gesi, Lusano Aibua Ubunifu wa Nishati Safi
Makala

Maji Yageuka Gesi, Lusano Aibua Ubunifu wa Nishati Safi

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
5 Min Read
Na Lucy Ngowi
WAKATI Tanzania ikiendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, mbunifu Lusano Luvanda, wa mradi wa Atlas, amebuni mashine inayozalisha gesi kupitia mchakato unaotumia maji, akilenga kutoa teknolojia inayoweza kutumika katika maeneo mbalimbali na kuchangia upatikanaji wa nishati safi.
Ubunifu huo ni miongoni mwa kazi zilizopata nafasi kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), katika kipindi ambacho taasisi hiyo inaadhimisha miaka 40 ya kukuza sayansi, teknolojia na ubunifu nchini.
Kwa Luvanda, safari ya ubunifu huo sasa imefika hatua muhimu ya kuutambulisha kwa jamii na kuandaa mazingira ya kuupeleka sokoni.
Anasema mashine hiyo huzalisha gesi pale inapohitajika na inaweza kutumika kwa majiko yanayotumia gesi, tofauti na mifumo ambayo mtumiaji hutegemea gesi iliyohifadhiwa tayari kwenye mtungi.
“Mtu anapohitaji gesi, mashine inazalisha. Akitumia na gesi ikaisha, mashine inazimwa. Akihitaji tena, anaianzisha na uzalishaji unaendelea,” anasema.
Kwa mbunifu huyo, moja ya malengo makubwa ya ubunifu huo ni kuchangia jitihada za Tanzania za kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Anasema mfumo huo hutumia maji katika mchakato wa uzalishaji wa gesi, ambayo hutumika kwenye moto na baada ya matumizi kutoa mvuke wa maji.
“Changamoto kubwa kwenye nishati ya kupikia ni moshi, masizi na uchafuzi wa hewa. Hapa tunatumia maji, gesi inakwenda kwenye moto na mwisho inazalisha tena mvuke wa maji,” anasema.
Habari Picha 13389
Ikiwa teknolojia hiyo itathibitishwa na kukidhi viwango vinavyohitajika kwa matumizi ya kibiashara, inaweza kuwa na manufaa kwa watumiaji wanaotafuta njia mbadala za nishati ya kupikia.
Kwa mfano, kaya, wafanyabiashara wa chakula na watumiaji wengine wanaotegemea gesi wanaweza kunufaika na mfumo unaolenga kuzalisha gesi wakati wa matumizi, badala ya kutegemea kuhifadhi kiasi kikubwa cha gesi kwa matumizi ya baadaye.
Pia, kwa kuwa mashine hiyo imetengenezwa kwa ukubwa tofauti, Luvanda anaamini inaweza kutumika katika mazingira mbalimbali kulingana na mahitaji ya mtumiaji.
Mbali na matumizi yake, Luvanda anasisitiza umuhimu wa kutengeneza teknolojia ndani ya nchi.
Anasema sehemu kubwa ya vifaa vinavyotumika kutengeneza mashine hiyo hupatikana na kufanyiwa kazi nchini, ikiwamo alumini na vifaa vingine vinavyotumika kuunda mfumo huo.
“Tunatengeneza hapa hapa. Hakuna kwamba tunachukua mashine nzima nje. Vifaa tunavitengeneza hapa na kuunganisha mfumo wenyewe,” anasema.
Kwa mtazamo huo, ubunifu huo unaweza kutoa fursa ya kujenga uwezo wa ndani katika utengenezaji wa teknolojia, huku hatua ya kuingia sokoni ikiwa na uwezo wa kufungua nafasi nyingine za uzalishaji na biashara.
Luvanda anasema alifikia hatua ya kuonyesha ubunifu wake kupitia mashindano yaliyompa fursa ya kuwasilisha kazi hiyo, kuchambuliwa na hatimaye kuchaguliwa miongoni mwa washindi waliopata nafasi ya kushiriki maonesho.
Habari Picha 13391
Anasema msaada wa tume hiyo umemsaidia zaidi katika hatua ya kuutambulisha ubunifu wake kwa umma.
“Kwa sasa COSTECH imenisaidia kujitambulisha, watu wajue zaidi kuhusu kazi yangu kwa sababu hii ni mara yangu ya kwanza kutoka nayo hadharani,” anasema.
Hata hivyo, anasema hatua inayofuata ni kuifikisha teknolojia hiyo sokoni, akilenga kuanza kufanya hivyo Desemba 2026, huku akitarajia kupata msaada zaidi wa kitaalamu na kibiashara.
“Tunatarajia kuingia sokoni Desemba. Tunahitaji msaada zaidi wa kutufikisha sokoni na pia msaada wa kiteknolojia ili tuweze kuendeleza kazi hii,” anasema.
Luvanda anatoa picha ya namna safari ya miaka 40 ya tume hiyo inaweza kuonekana kupitia wabunifu wanaotafuta majibu ya changamoto za jamii.
Kwa Luvanda, fursa hiyo haijampa tu jukwaa la kuonyesha mashine yake, bali pia imeanza kumtoa katika hatua ya kuwa na wazo na kumpeleka kwenye hatua ya kulitambulisha kwa watumiaji na kutafuta soko.
Safari bado ni ndefu, lakini lengo lake ni wazi, kuona teknolojia inayotengenezwa na mbunifu wa Kitanzania ikitoka kwenye maonesho na kufika katika maisha ya kila siku ya wananchi.
Hapo ndipo miaka 40 ya tume hiyo inapopata sura halisi si katika idadi ya miaka pekee, bali katika wabunifu wanaopewa nafasi ya kubadili mawazo yao kuwa teknolojia zenye kutafuta majibu ya changamoto za jamii.

You Might Also Like

Madaktari Toka China Waleta Matumaini Barani Afrika

Utafiti wa Chakula Bora cha Kuku wa Nyama Watoa Tumaini kwa Wafugaji

Ujenzi Wa Maabara Tatu Za Sayansi Kuanza, OUT Yasaini Mkataba

Miaka 40 ya Costech: Ruzuku ya Ubunifu Imegeuza Wazo Kuwa Kiwanda Cha Kimataifa

Mawasiliano Kati ya China, Afrika Juu Ya Mtazamo Wa Maandishi Ya Kifasihi

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Bunifu Ya Dawa Ya Mayai Kupunguza Hasara Kwa Wafugaji Wa Kuku
Next Article Dkt Yonaz Awakumbusha Vijana Kulinda Afya Zao Katika Mapambano Dhidi Ya Ukimwi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Bunifu ya dawa ya mayai yapunguza hasara kwa wafugaji wa kuku
Makala August 22, 2026
Dkt Yonaz Awakumbusha Vijana Kulinda Afya Zao Katika Mapambano Dhidi Ya Ukimwi
Habari August 22, 2026
Bunifu Ya Dawa Ya Mayai Kupunguza Hasara Kwa Wafugaji Wa Kuku
Makala August 22, 2026
TTCL Yazindua Awamu Ya Pili,’Faiba Mlangoni Kwako’ Yasisitiza Kupanua Wigo Wa Huduma
Habari August 22, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?