MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Maabara Za TARURA Nguzo Ya Ubora Wa Miradi Ya Barabara Na Madaraja Nchini
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Maabara Za TARURA Nguzo Ya Ubora Wa Miradi Ya Barabara Na Madaraja Nchini
Habari

Maabara Za TARURA Nguzo Ya Ubora Wa Miradi Ya Barabara Na Madaraja Nchini

Author
By Author
Share
2 Min Read
‎Na Lucy Lyatuu
‎WAKALA wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) umeendelea kuimarisha usimamizi wa ubora wa miradi ya ujenzi wa miundombinu nchini kupitia maabara zake za kisasa zinazofanya uchunguzi na uhakiki wa vifaa vya ujenzi pamoja na kazi zinazotekelezwa hatua inayochangia kujenga miundombinu imara, salama na yenye kudumu kwa muda mrefu.
‎
‎Akizungumza katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), Fundi Sanifu kutoka Kitengo cha Utafiti na Udhibiti Ubora TARURA Makao Makuu, Jacob Manguye amesema maabara hizo zina jukumu muhimu la kuhakikisha miradi yote ya barabara, madaraja na miundombinu mingine inazingatia viwango vya kitaalamu na masharti ya mikataba kabla na baada ya utekelezaji.
Habari Picha 12764
‎
‎Amesema wataalamu wa maabara hufanya vipimo vya kina vya vifaa vya ujenzi kabla havijatumika kwenye miradi sambamba na kuhakiki ubora wa kazi zinazotekelezwa na wakandarasi ili kuhakikisha zinakidhi viwango vinavyotakiwa.
‎
‎”Tunafanya uhakiki wa kazi mbalimbali ikiwemo za vifusi, lami, madaraja na miundombinu mingine ili kuhakikisha miradi inayotekelezwa inakuwa na ubora wa hali ya juu na inadumu kwa muda mrefu”, amesema Manguye.
‎
‎Amebainisha kuwa kwa sasa TARURA ina maabara kuu iliyopo Makao Makuu Dodoma pamoja na maabara nyingine 14 zilizosambazwa katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Kigoma, Arusha na Moshi. Maabara hizo zinatoa huduma za upimaji wa vifaa vya ujenzi na uhakiki wa ubora wa miradi kwa lengo la kuongeza ufanisi na thamani ya fedha katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
‎
‎Mbali na hilo, amesema TARURA inamiliki mtambo maalumu wa uchunguzi wa udongo (Geotech) unaowezesha kufanya tafiti za kina kuhusu uwezo wa udongo kuhimili ujenzi wa madaraja, majengo na miundombinu mingine mikubwa kabla ya ujenzi kuanza hatua inayosaidia kupunguza hatari za uharibifu wa miundombinu na kuongeza usalama wa watumiaji.
‎
‎Manguye ametoa wito kwa wakandarasi, wahandisi, taasisi za ujenzi na wadau wengine wa sekta hiyo kutumia huduma za maabara za TARURA ili kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa inafikia viwango vinavyotakiwa na kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.
  • Habari Picha 12765

You Might Also Like

DCF Atembelea Banda Wizara Mambo YA Nje, Atoa Pongezi

Mita  Janja Zazinduliwa,  Tanesco  Yatakiwa Kuzisambaza Nchi Nzima

MOI Yatoa Huduma Mpya Bobezi Tisa Kwa Mwaka 2025 

Umwagiliaji kumwezesha mkulima kulima mara mbili mpaka tatu kwa mwaka

Simbachawene Ashauri Suluhu ya Mafuriko Mpwapwa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article AGITF Kutekeleza Dira Kwa Kasi Kwa Kuwezesha Wakulima Kunufaika Na Mikopo Ya Bei Nafuu
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

AGITF Kutekeleza Dira Kwa Kasi Kwa Kuwezesha Wakulima Kunufaika Na Mikopo Ya Bei Nafuu
Habari July 10, 2026
Ziwa Ngozi Lavuta Mamia Sabasaba, Wageni Washangazwa Na Ramani Ya Afrika Juu Ya Mlima
Habari July 9, 2026
Shirika La Uzalishaji Mali La Polisi Kujenga Vituo Vya Ukaguzi Wa Vyombo Vya Moto
Habari July 9, 2026
Watumishi 7881 Watakaostaafu 2026/27 Watambuliwa Kupitia Kampeni Ya Tunalipa Jana-PSSF
Uncategorized July 8, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?