MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Askofu Chilongani Aitaka Jamii Kutumia Ijumaa Kuu Kusameheana na Kujenga Umoja
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Askofu Chilongani Aitaka Jamii Kutumia Ijumaa Kuu Kusameheana na Kujenga Umoja
Habari

Askofu Chilongani Aitaka Jamii Kutumia Ijumaa Kuu Kusameheana na Kujenga Umoja

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Mwandishi wetu
DODOMA: ASKOFU wa Kanisa Anglikana Tanzania, Dayosisi ya Central Tanganyika, Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu, Dkt. Dikson Chilongani, ameitaka Serikali na Watanzania kwa ujumla kuitumia siku ya Ijumaa Kuu kama fursa ya kusameheana na kuacha nyuma changamoto zilizopita.
Akizungumza Aprili 3, 2026, katika ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika kanisani hapo, Askofu Chilongani amesema siku hiyo, inayokumbuka mateso na kifo cha Yesu Kristo, inapaswa kuwa chachu ya upendo, umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi.
Amesisitiza kuwa viongozi wa Serikali na wa dini wanapaswa kutumia nafasi zao kuimarisha umoja wa kitaifa kwa kuondoa chuki, ubinafsi na migawanyiko isiyo na tija.
Habari Picha 11676
Amebainisha kuwa ni muhimu kwa viongozi hao kuonesha mfano kwa kusameheana na kuweka mazingira yatakayowezesha wananchi kuishi kwa amani.
“Tumepitia changamoto mbalimbali katika kipindi kilichopita, hivyo ni wakati wa kuziachilia na kuanza ukurasa mpya wa upendo na mshikamano kwa ajili ya ustawi wa taifa,” amesema.
Aidha, Askofu Chilongani ameeleza kuwa msamaha si wa viongozi pekee, bali ni jukumu la kila Mtanzania, kwani ni tendo la kiroho linalochangia kujenga jamii yenye maelewano na utulivu.
Katika mahubiri hayo, ameongeza kuwa taifa lenye afya linahitaji viongozi na wananchi wanaojali, wanaosikilizana na wanaoepuka chuki pamoja na ubinafsi.
Wakati huo huo, Mchungaji Adrian Mdao, akisoma somo la tano kati ya masomo saba, amesisitiza umuhimu wa kusikiliza sauti za wenye uhitaji.
Amesema baadhi ya wazazi na watumishi wa umma wamekuwa wakipuuza wajibu huo kutokana na majukumu au kutokuwa tayari kusikiliza changamoto za wengine.
Habari Picha 11677
Ametoa wito kwa walio na mamlaka kutumia nafasi zao kusaidia badala ya kuumiza, akisisitiza kuwa kusikiliza na kujibu mahitaji ya watu ni msingi wa kujenga jamii yenye upendo, kuaminiana na mshikamano.

You Might Also Like

OCPD Yakabidhi Juzuu Mpya za Sheria kwa Ofisi ya Taifa ya Mashitaka

Ukosefu wa Chakula Shuleni Waathiri Wanafunzi Longido, CORDS Waja na Mrad

Katambi Awataka CBE Kutoa Elimu Yenye Ushindani Kimataifa

TFRA yazindua Chama cha wafanyabiashara wa Mbolea

Tumeridhika na kazi za TTCL – Mwanaisha

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TAWIA na MAIPAC washirikiana kuadhimisha Siku ya Wajane, wapanga kupanda Mlima Kilimanjaro
Next Article Serikali Yaanza Mikakati Ya Kukabiliana Na Wanyamapori Wakali, Waharibifu
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NIDA Kufanya Usajili Wa Watoto  Kuanzia Umri Wa Kuzaliwa,Kutoa Namba Maalum
Habari May 25, 2026
TPHPA Yatumia Mbinu za Kibaiolojia Kudhibiti Gugu Ziwa Victoria
Habari May 24, 2026
Wizara Ya Viwanda Kutekeleza Vipaumbele Saba, Ipo  Miradi Ya Viwanda Ya  Kimkakati
Habari May 22, 2026
Biashara 15 Hazitakiwi Kufanywa Na Wageni Ndani Ya Nchi
Habari May 22, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?