MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Taska Mbogo Aitaka Serikali Kurejesha Viwanda, Kuimarisha Kilimo
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Taska Mbogo Aitaka Serikali Kurejesha Viwanda, Kuimarisha Kilimo
Habari

Taska Mbogo Aitaka Serikali Kurejesha Viwanda, Kuimarisha Kilimo

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: MBUNGE wa Viti Maalum, Taska Mbogo, amesema Serikali imekuja na mpango mzuri wa Dira ya Maendeleo 2050, unaolenga kuhakikisha Tanzania inafikia hadhi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2050.
Ameeleza hayo bungeni jijini Dodoma, alipokuwa akichangia mipango ya utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050.
Amesema lengo kuu ni kuwa na viwanda vya kutosha vitakavyowezesha uzalishaji wa bidhaa kwa ajili ya matumizi ya ndani na kuuza nje ya nchi.
Ameeleza kuwa ujenzi wa viwanda nchini si jambo jipya, kwani hapo awali kulikuwapo viwanda vingi ikiwemo vya nguo kama Mutex, Mwatex, Urafiki na Kilitex, ambavyo vilitumia malighafi ya pamba inayozalishwa nchini,
Hata hivyo, viwanda hivyo kwa sasa havifanyi kazi kutokana na sera ya ubinafsishaji.
Amesema kuwa wakati huo ubinafsishaji ulikuwa ni lazima, lakini kwa sasa viwanda vingi vilivyobinafsishwa havifanyi kazi.
Ameomba Serikali ivichukue tena ili wakulima waweze kupata soko la uhakika la pamba.
Aidha, amesema kulikuwapo pia viwanda vya kusindika nyama kwa ajili ya kuuza nje ya nchi, viwanda vya mafuta na jumla ya viwanda takribani 364 vilivyobinafsishwa.
Ameomba Serikali ipitie upya mikataba ya ubinafsishaji ili kuona uwezekano wa kuvirejesha.
Kwa upande wa kilimo, ameishauri Serikali kuwekeza zaidi kwani ndicho uti wa mgongo wa uchumi.
Ameeleza kuwa wakulima wengi hupata hasara kutokana na gharama kubwa za uzalishaji, hususan mbegu na mbolea.
Amehoji kwanini mbegu za mahindi zinazozalishwa sasa haziwezi kupandwa tena, tofauti na mbegu za asili.
Ameomba watafiti wa kilimo wafanye utafiti ili kurejesha mbegu zitakazomsaidia mkulima kujiendesha bila gharama kubwa.
Kuhusu utalii, amesema filamu ya ‘Royal Tour’ imeongeza mapato, hivyo Serikali iendelee kuwekeza katika kuboresha miundombinu ya hifadhi ili kuvutia watalii wengi zaidi.

You Might Also Like

Zabibu Ya Makutupora Nyekundu Yatajwa Kuwa Ya Kipekee Duniani

Maabara Ya Mkemia Mkuu Yashauri Wajasiriamali Wa Kemikali

OSHA Yatoa Gawio Kwa Serikali Zaidi  Ya Bilioni 10

Rais Samia Kushiriki Mkutano Wa Wakuu Wa Nchi Ethiopia

Waziri Mkuu Majaliwa Amwakilisha Dkt.Mpango Mahafali Ya 43 OUT

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Makampuni 408 Ya Tanzania Yaruhusiwa Kusafirisha Mazao Ya Kilimo Kwenda China
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Makampuni 408 Ya Tanzania Yaruhusiwa Kusafirisha Mazao Ya Kilimo Kwenda China
Habari February 5, 2026
Serikali Yaweka Utaratibu Biashara Pembezoni mwa Barabara
Habari February 5, 2026
TEHAMA Kuchochea Uchumi wa Kidijitali, Serikali Yatenga Sh Bil Tano Kwa Kampuni Changa
Habari February 5, 2026
Wananchi wa Bukoba Wapewa Vizimba vya Samaki Kuongeza Mapato
Habari February 4, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?