MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Mbunge Mgalu Auliza Hatima ya Ujenzi wa Chuo cha VETA Bagamoyo
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Mbunge Mgalu Auliza Hatima ya Ujenzi wa Chuo cha VETA Bagamoyo
Habari

Mbunge Mgalu Auliza Hatima ya Ujenzi wa Chuo cha VETA Bagamoyo

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
MBUNGE wa Jimbo la Bagamoyo (CCM), Subira Mgalu, ameuliza swali bungeni akitaka kufahamu iwapo Serikali ipo tayari kutenga fedha katika mwaka wa fedha 2026/2027 kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) katika wilaya hiyo.
Akiuliza swali hilo, Mbunge Mgalu amesema Halmashauri ya Bagamoyo tayari imetenga eneo na kulikabidhi kwa Mamlaka ya VETA kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho.
Ameongeza kuwa ujenzi wa chuo hicho pia umeainishwa katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Habari Picha 10985
“Kwa kuwa Halmashauri ya Bagamoyo imetenga eneo na kulikabidhi VETA kwa ajili ya ujenzi wa chuo, na jambo hili lipo kwenye Ilani ya CCM,
“Je, Serikali ipo tayari kutenga fedha katika mwaka huu wa fedha 2026/2027 ili vijana wa Bagamoyo wapate stadi mbalimbali
 zitakazowawezesha kushiriki katika miradi ya kimkakati inayotarajiwa kutekelezwa, ikiwemo ujenzi wa bandari?” alihoji Mbunge Mgalu.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wanu Ameir, amesema kuwa Serikali katika mwaka wa fedha 2024/2025 ilitenga Sh. Bilioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa awali wa vyuo vya VETA nchini.
Aliongeza kuwa kwa mwaka wa fedha 2025/2026, Serikali tayari imetenga Sh. Bilioni 21.262 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa awamu ya kwanza, pamoja na kuanza ujenzi wa vyuo vya VETA katika maeneo ambayo bado hayana vyuo hivyo.

You Might Also Like

Rais Samia afungua kikao kazi cha watendaji serikalini

TUCTA Yakutana Na Mkuu Wa Mkoa Mbeya, Maandalizi Mei Mosi kitaifa 2025.

Waziri Sangu Aagiza Hatua Kali kwa Waajiri Wanaokwepa Kuwasilisha Michango NSSF

Kadi za mpiga kura zenye jina la zamani la Tume ni halali

Bonifas Jacob aahidi  akishinda Uenyekiti Kanda ya Pwani hatakaa ofisini

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Serikali Yachukua Hatua Madhubuti Kukuza Ajira kwa Wahitimu wa Vyuo
Next Article Mvua, Upepo Yaharibu Shule Lindi, Serikali Yatoa Milioni 96
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Sheria Ya  Kuzuia Shisha Kutungwa, Yabainika Kuwekwa Dawa Za Kulevya
Habari May 29, 2026
Waraibu Wa Dawa Za Kulevya 85,425  Wapatiwa Huduma Ya Tiba Nchini Kwa Mwaka 2025
Habari May 29, 2026
NHC Kuendelea Kutekeleza Miradi Mikubwa Ya Kimkakati Ya Ujenzi Wa Nyumba
Habari May 28, 2026
Kutokulipa Kodi Ya Pango La Ardhi Unakosa Sifa Za Kugombea Nafasi Za Uongozi
Habari May 28, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?