MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Dkt. Majule Ahoji Hatua za Kulinda Wananchi Dhidi ya Mikopo Hatari
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Dkt. Majule Ahoji Hatua za Kulinda Wananchi Dhidi ya Mikopo Hatari
Habari

Dkt. Majule Ahoji Hatua za Kulinda Wananchi Dhidi ya Mikopo Hatari

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
MBUNGE wa Viti Maalum, Dkt. Neema Majule, amehoji Serikali kuhusu hatua zinazochukuliwa kudhibiti mikopo hatarishi yenye riba kubwa inayotolewa na taasisi zisizo rasmi nchini.
Dkt. Majule aliuliza swali hilo Bungeni jijini Dodoma akitaka kufahamu mikakati ya Serikali ya kulinda wananchi dhidi ya mikopo hiyo inayowaathiri kiuchumi.
“Je, Serikali imechukua hatua gani kudhibiti mikopo hatarishi yenye riba kubwa zinazotolewa na baadhi ya taasisi zisizo rasmi?” alihoji Dkt. Majule.
Akijibu, Naibu Waziri wa Fedha, Laurent Luswetula, alisema kuwa Serikali, kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, imechukua hatua kadhaa za kudhibiti mikopo hiyo.
Alibainisha kuwa hatua hizo ni pamoja na kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kupata mikopo kutoka kwa watoa huduma wenye leseni, kama inavyotakiwa na Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006 na Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018.
Naibu Waziri Luswetula pia alisema kuwa Serikali imewatambua na kuchukua hatua za kiutawala dhidi ya watoa mikopo wasioidhinishwa, huku jumla ya programu 69 za mikopo ya kidigitali zilizokuwa zikitoa mikopo bila leseni zikisitishwa na programu nyingine 126 kufungiwa.
“Pia, Serikali imetoa mwongozo maalum kwa watoa huduma za mikopo ya kidigitali ili kuhakikisha uwazi, uendeshaji wa kimaadili, utoaji wa taarifa kamili kuhusu gharama za mikopo na ulinzi wa watumiaji wa huduma za kifedha,” alisema.
Aliongeza kuwa Serikali tayari imeandaa rasimu ya kanuni za kusimamia mikopo ya kidigitali, ambazo zinatarajiwa kuanza kutumika katika mwaka wa fedha 2026/2027, kwa lengo la kuimarisha udhibiti wa wakopeshaji wa kidigitali nchini.

You Might Also Like

TPHPA Yaimarisha Mapambano Dhidi Ya Visumbufu Vya Mazao

Maabara Ya Mkemia Mkuu Yashauri Wajasiriamali Wa Kemikali

Muswada wa Kuwalinda Wafanyakazi wa Ndani Waja

Rais Samia Ni Mama Wa Maendeleo – Majaliwa

UDSM  Kujenga Jengo La Kisasa La Bil 8.3

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TPHPA Yapata Tuzo ya WCO kwa Ulinzi wa Afya na Usalama wa Taifa
Next Article MBUNGE wa Kasulu Mjini Ahoji Serikali Kuhusu Mradi wa Maji Mwanga B
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

VETA kumpa nafasi Igobeko kuongeza ujuzi na kuwawezesha wengine
Habari August 23, 2026
Airtel Yajenga Darasa La Fursa Katika Shule Ya Sekondari Magaoni,Tanga
Habari August 23, 2026
Bunifu ya dawa ya mayai yapunguza hasara kwa wafugaji wa kuku
Makala August 22, 2026
Dkt Yonaz Awakumbusha Vijana Kulinda Afya Zao Katika Mapambano Dhidi Ya Ukimwi
Habari August 22, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?