MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Nishati Safi Ya Rafiki Briquettes Iwafikie Watanzania Wote-Balozi Kingu
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Nishati Safi Ya Rafiki Briquettes Iwafikie Watanzania Wote-Balozi Kingu
Habari

Nishati Safi Ya Rafiki Briquettes Iwafikie Watanzania Wote-Balozi Kingu

Author
By Author
Share
3 Min Read

Na Mwandishi Wetu

WATANZANIA  wametakiwa kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kutumia nishati safi ya kupikia (mkaa mbadala wa Rafiki briquettes) unaozalishwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).

Rai hiyo imetolewa leo Januari 24, 2026 na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Meja Jenerali Mstaafu  Balozi Jacob Kingu akiwa ameambatana na Wajumbe wa REB na Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) walipotembelea kiwanda cha Nishati safi ya Rafiki Briquettes kinachomilikiwa na STAMICO kilichopo Kisarawe Mkoani Pwani.

Habari Picha 10934

Balozi Kingu amewataka STAMICO kuongeza kasi ya uzalishaji wa mkaa wa Rafiki briquettes ili watanzani wote nchini waweze kutumia nishati safi ya kupikia na salama.

“Hii ajenda ya matumizi ya nishati safi ambayo kinara wake ni Rais wa Awamu ya Sita, Dkt. Samia Suluhu Hassan inalenga kumkomboa Mwanamke ili aachane na matumizi ya nishati isiyo safi na salama. Tunahamasisha na kutekeleza maono haya ya Kiongozi wetu”, amesema Balozi Kingu

Habari Picha 10935

Ameongeza kuwa, ushirikiano wa REA na STAMICO katika Kutekeleza Miradi ya Nishati Safi ya Kupikia umelenga kufikia asilimia 80 ifikapo mwaka 2034 (Mkakati 2024-2034).

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa REA,  Hassan Saidy ameongeza kuwa Wakala unaendelea kushirikiana na Wadau mbalimbali ili kuhakikisha Mkakati wa Nishati safi ya kupikia unatimiza malengo yaliyowekwa, ikiwa ni pamoja na kuongeza upatikanaji na usambazaji wa mkaa mbadala.

Habari Picha 10936

Naye, Sophia Mgonja Mjumbe wa Bodi ya REB amewapongeza STAMICO kwa namna wanavyotengeneza mkaa mbadala katika kiwanda hicho cha Nishati safi cha Rafiki briquettes na kuwataka wadau mbalimbali kutumia nishati safi hiyo inayozalishwa ili kuifanya ajenda ya nishati safi kuwa endelevu na kuwafikia watanzania wengi.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa STAMICO  Baraka Manyama amesema kuwa mradi wa Rafiki Briquettes  umesaidia katika utunzaji wa mazingira (umeokoa majanga ya kimazingira), pia umekua chanzo kikubwa cha ajira kwa makundi mbalimbali wakiwemo wanawake, vijana na wadau mbalimbali.

Habari Picha 10937

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na Shirika la Taifa la Madini (STAMICO) wamesaini mkataba wa kujenga kiwanda kipya cha kuzalisha nishati mbadala (Mkaa mbadala wa Rafiki Briquettes) mkoani Geita ambapo mkataba huo una thamani ya sh bilioni 4.5 na ujenzi unaemdelea.

You Might Also Like

Ridhiwani Awashika Mkono Wenye Mahitaji Maalum

Rais Samia Kuzindua Mfuko wa Mikopo Wenye Kianzio Cha Sh. Bilioni 2.3

CMA Inasaidia Vijana Kuwa Na Nafasi Bora Kazini

Mwenyekiti TCCIA Geita Gabriel Ahamasisha Watanzania Kutumia Bidhaa Za Ndani

Wachimbaji Wadogo Wafikiwa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Bil 67 Zatumika Kujenga Barabara, Masoko  Mwanza-Profesa Shemdoe
Next Article Sekta Ya Madini Yazidi Kupaa,  Mchango Wake Kwa Pato La Taifa Waongezeka 
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mbunge Asisitiza Sheria za Majiko Safi Ili Kulinda Mazingira
Habari February 3, 2026
Mwalunenge: Bila Rasilimali Watu Na Mtaji, Mipango Ya Kilimo Haitafanikiwa
Habari February 3, 2026
Gulamali Ahoji Bungeni Changamoto ya Mawasiliano Ilongelo
Makala February 3, 2026
Serikali Yaendelea Kuimarisha Uhuru wa Mahakama – Nchimbi
Habari February 2, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?