MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Bil 67 Zatumika Kujenga Barabara, Masoko  Mwanza-Profesa Shemdoe
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Bil 67 Zatumika Kujenga Barabara, Masoko  Mwanza-Profesa Shemdoe
Habari

Bil 67 Zatumika Kujenga Barabara, Masoko  Mwanza-Profesa Shemdoe

Author
By Author
Share
2 Min Read

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

WAZIRI  wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI)  Profesa Riziki Shemdoe amesema Serikali kupitia Mradi wa Uendelezaji Miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) imetumia kiasi cha  Sh. bilioni 67 kujenga Barabara na Masoko ili kuwahudumia wananchi wa Mwanza.

Profesa Shemdoe ametoa taarifa hiyo alipopewa nafasi na Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba ya kuzungumza na wananchi wa Mwanza waliojitokeza kumsikiliza mara baada ya  kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo na kuzindua meli ya New MV Mwanza.

Profesa Shemdoe amefafanua kuwa, fedha hizo zinatumika kujenga barabara ya Nyamaghana yenye urefu wa kilomita 14 yenye thamani ya Sh  Bilioni 22, barabara ya Ilemela yenye urefu wa kilomita 12 yenye thamani ya Sh Bilioni 24, soko la samaki Mkuyuni Nyamaghana lenye thamani ya Sh Bilioni saba  pamoja na soko la mazao mchanganyiko Ilemela lenye thamani ya Sh Bilioni 14.

Habari Picha 10930

Akizungumzia hatua ya ujenzi wa barabara hizo, Profesa Shemdoe amesema zimekamilika na ziko kwenye hatua ya kuweka taa za barabarani ili wananchi waweze kuzitumia nyakati za usiku huku wakiwa salama.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu ikikupendeza pindi barabara zikikamilika, tutakuomba uje kuzizindua rasmi kwa ajili ya kuanza kutumiwa na wananchi wa Mwanza na watanzania wote watakaokuja Jijini Mwanza kwa shughuli mbalimbali,” Profesa Shemdoe amewasilisha ombi.

Profesa  Shemdoe amemhakikishia Waziri Mkuu  kuwa, ofisi yake itaisimamia vema TARURA ili miradi yote ya barabara, soko la samaki na soko la mazao mchanganyiko ikamilike kwa wakati, na hatimaye wanachi waanze kunufaika na uwepo wa miradi hiyo.

You Might Also Like

CCCC Yagusa Wanafunzi Msasani kwa Msaada wa Vifaa vya Shule, Chakula

Tido Mhando: Marufuku Kuwasilisha Vyeti, Nyaraka Za Kughushi Maombi ya Ithibati, Press Card

Dar es Salaam Kuunda Kamati Ya Kupitia Majengo Chakavu

Waziri Sangu Aagiza Hatua Kali kwa Waajiri Wanaokwepa Kuwasilisha Michango NSSF

Maandalizi Mei Mosi Yapamba Moto Singida

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Kiwanda cha Sukari Mkulazi Chaanza Kuleta Tija, Sangu Apongeza Uwekezaji wa NSSF na Magereza
Next Article Nishati Safi Ya Rafiki Briquettes Iwafikie Watanzania Wote-Balozi Kingu
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Wananchi Washauriwa Kutumia  Wataalam Wa Ujenzi Kuepuka Madhara
Habari July 14, 2026
July 14, 2026
Uncategorized July 14, 2026
TANESCO Kutambulisha Mfumo Wa Kufunga Nyaya Kwenye Nyumba Ukifuatilia Matumizi Ya Umeme
Habari July 13, 2026
Wananchi Waendelea Kunufaika Na Ofa Za TTCL Sabasaba 2026
Habari July 13, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?