MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Uwekezaji Mkubwa Uliofanywa Na Serikali, Kituo Cha Gesi Asilia Mlimani Waleta Nafuu Kwa Wananchi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Uwekezaji Mkubwa Uliofanywa Na Serikali, Kituo Cha Gesi Asilia Mlimani Waleta Nafuu Kwa Wananchi
Habari

Uwekezaji Mkubwa Uliofanywa Na Serikali, Kituo Cha Gesi Asilia Mlimani Waleta Nafuu Kwa Wananchi

Author
By Author
Share
4 Min Read

 

Na Mwandishi  Wetu

NAIBU  waziri wa  Nishati Salome Makamba ameeleza kuwa, Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika kujenga kituo cha kujaza gesi asilia kwenye vyombo vya usafiri katika eneo la Mlimani jijini Dar es Salaam ambapo zaidi ya sh.Bilioni 12 zimetumika kukamilisha kituo hicho chenye uwezo wa kuhudumia magari madogo na bajaji 800 kwa siku.

 

Salome amebainisha hayo Novemba 12, 2025 Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kukagua kituo hicho kinachosimamiwa na Kampuni Tanzu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC) ya GASCO.

 

Salome ameeleza kuwa Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassan inahakikisha rasilimali zilizopo zinawanufaisha wananchi kwa namna mbalimbali.

Habari Picha 10564

 

“Matumizi ya gesi asilia iliyoshindiliwa (CNG) yamerahisisha gharama za maisha kwa watu wa vyombo vya usafiri kwani gharama ya gesi kilo moja ni shilingi 1500 ambapo ukiwa na mtungi wa Kilo 17 unaweza kusafiri umbali wa KM 50 hii inaonesha dhahiri kuwa gesi inagharama nafuu zaidi kuliko mafuta lakini pia kutokana na wingi wa magari ya biashara na bajaji  katika mkoa wa Dar es Salaam uwekezaji huu umekuwa ni fursa kwa wafanyabiashara hao katika kupunguza gharama za uendeshaji na kuongeza kipato.” Amesema Salome

 

Ameeleza kuwa, hadi kufikia Juni 2026 kutakuwa na vituo vingine vya kujaza gesi katika maeneo ya kila  barabara kubwa  ya Mkoa wa Dar es Salaam huku akisisitiza kuwa Serikali pia imeanza mpango wa kujenga vituo vikubwa katika Mikoa ya Morogoro, Dodoma, Arusha, Kilimanjaro na Tanga ambavyo vitasaidia wananchi wa mikoa hiyo kupata huduma lakini pia wananchi wa Mikoa ya karibu kunufaika na huduma husika.

Habari Picha 10565

 

Salome ametoa wito kwa sekta binafsi kuongeza kasi ya uwekezaji katika miundombinu ya gesi asilia, akibainisha kuwa mahitaji ya nishati nafuu yanaongezeka kwa haraka nchini hivyo ni fursa kwao kuwekeza ili kurahisisha upatikanaji wa nishati hiyo kwani Serikali imeboresha mazingira ya uwekezaji kupitia mfumo wa ushirikishwaji wa Biashara kati ya Serikali na sekta binafsi (PPP) hasa kupitia mfumo wa One Stop Centre ambao ni rahisi kufikisha huduma kwa wananchi.

 

Pamoja na hilo amesisitiza kuwa Serikali inaendelea kutoa kipaumbele kwa vijana kwani sekta ya gesi na mafuta inawagusa moja kwa moja vijana wanaofanya biashara za bolt na bajaji kwani gharama za uendeshaji ni nafuu zaidi.

Habari Picha 10566

 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC,  Mussa Makame ameeleza kuwa kituo cha kujaza gesi Mlimani  kina uwezo wa kujaza hadi kilogrmu  70,000 lakini kwa sasa kinajaza hadi kilogramu 50 kwa bajaji, magari madogo pamoja na magari makubwa.

 

“Zamani kabla ya kujengwa kwa kituo hiki cha Serikali wananchi walikuwa wakijaza gesi katika vituo binafsi ambapo walikuwa wakitumia masaa matatu lakini kwa sasa gari zinatumia dakika nne kujaza gesi na kwa siku kinajaza magari madogo na bajaji 800 lakini magari makubwa 15 yanayopeleka gesi katika vituovidogo.

 

Amesema  kwa kushirikiana na Sekta binafsi Serikali itahakikisha kufikia 2026 Dar es Salaam inakuwa na vituo vikubwa 15 vya kujaza gesi lakini pia Mikoa ya Pwani, Morogoro, Dodoma, Arusha, Kilimanjaro na Tanga.

Habari Picha 10567

 

 

Nao wanufaika wa gesi asilia wameishukuru Serikali kwa kuanzisha mradi huo pamoja na  kuendelea kuboresha miundombinu kwani mwanzoni walikuwa wakitumia muda mrefu kujaza gesi lakini kwa sasa wanajaza na kuondoka kwa wakati hali inayowasaidia katika kupunguza gharama za uendeshaji na kuongeza kipato.

 

You Might Also Like

Maofisa Tarafa na Watendaji wa Kata Waaswa kuwa wabunifu

Ridhiwani: WCF Umeboresha Mifumo Ya Ushughulikiaji Wa Fidia

Wanawake Tumieni Fursa Zilizopo Kufanya Biashara

Rais Samia Awatega Wateule Wake

Chuo Cha VETA Chazindua Mradi Wa Biogas

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Spika Zungu Atangaza Kifo Cha Mbunge Wa Peramiho, Jenista Mhagama
Next Article Waomba Ajira 12,000 Kwenye Utumishi Wa Umma Kuanza  Kusailiwa  
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Waomba Ajira 12,000 Kwenye Utumishi Wa Umma Kuanza  Kusailiwa  
Habari December 12, 2025
Spika Zungu Atangaza Kifo Cha Mbunge Wa Peramiho, Jenista Mhagama
Habari December 11, 2025
Mkenda: Maendeleo ya Taifa Yanategemea Sayansi na Teknolojia
Habari December 11, 2025
Dkt. Ikomba wa CWT Aeleza Jinsi Elimu Ilivyobadilisha Taswira ya Tanzania kwa Miaka 64
Habari December 9, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?