Nenda moja kwa moja kwenye maudhui
November 5, 2026
Habari Author 14

NIDA Yapata Kibali Maalum Kurekebisha Taarifa Kwa Walioghushi Ili  Kujisajili

Na Lucy Lyatuu

MAMLAKA ya Vitambulisho Vya Taifa (NIDA) imesema serikali imetoa kibali maalum kwa ajili ya kushughulikia maombi  ya mabadiliko ya taarifa kwa waliotumia nyaraka za kughushi pamoja na waliotoa taarifa za udanganyifu walipojisajili kwa Mamlaka hiyo.

Imesema kibali hicho maalum kimetolewa kwa muda maalum wa mwaka mmoja na kwamba wenye changamoto za taarifa hizo kujitokeza na kwenda kwenye ofisi za NIDA za wilaya wakiwa na viambatanisho vinavyotakiwa ili kufanya marekebisho wanayohitaji katika muda uliopangwa.

Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, James Kaji amesema hayo Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa Habari na kuongeza kuwa kibali cha maombi hayo kinahusisha makundi mbalimbali  ikiwemo waathirika wav yeti  vya kughushi, waliofukuzwa katika ajira  za serikali kutokana na kutumia  vyeti vya shule  vya kugushi ambapo  pia walitumia vyeti hivyo kujisajili NIDA.

Imesema kundi lingine ni watu waliotumia majina ya watu wengone kupata elimu,watu wlaiotoa  taarifa za  uongo au udanganyifu katika usajili wa NIDA na raia wa Tanzania waliojisajili kama wakimbizi.

Kaji amewataka  wananchi wa makundi hayo kufika katika Ofisi za NIDA za wilaya wakiwa na nyaraka zinazohitajika ili kushughulikia maombi ya mabadiliko hayo.

Amesema watu hao watalazimika kuwa na viambatanisho vya  lazima Pamoja na vya ziada kama watakavyoelekezwa.

 

Habari Picha 10464

Amevitaja viambatanisho hivyo kuwa ni Pamoja na  nakala ya vyeti halisi vya elimu,cheti cha kuzaliwa  kilichohakikiwa na RITA Deep Pool  iliyosajiliwa na gazeti la serikali na nyaraka nyingine itakayotakiwa na Ofisi za NIDA.

Amesema maombi yatakayofanyiwa kazi ni yale yatakayokidhi masharti na vigezo vilivyowekwa baada ya wahusika kuwasilisha nyaraka zinazotakiwa  kwa ajili ya kuthibitisha taarifa zao.

Aidha Mamlaka hiyo imesema kwa kuwa kibali hicho kimetolewa kwa muda maalum, wale wenye changamoto za taarifa zao kujitokeza na kwenda  kwenye ofisi za NIDA za wilaya wakiwa na viambatanisho vinavyotakiwa ili kufanya marekebisho wanayohitaji katika muda uliopangwa.

Kadhalika inawaomba wananchi kutoa taarofa sahihi na za ukweli wanapokuwa wakijisajili NIDA kwa ajili ya  utambulisho wa taifa kw akuwa kutoa taarifa zisizo sahihi au kufanya udanganyifu wa taarifa wakati wa usajili ni kosa kwa mujibu wa sheria ya usajili na utambuzi wa watu.

 

 

Je, habari hii ilikusaidia?
Sambaza

Maoni 0

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!

Acha maoni

Barua pepe yako haitachapishwa. Sehemu zenye * ni lazima.