MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Madaktari Kutoka Ireland Watoa Matibabu Ya Mifupa Kwa Watoto MOI
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Madaktari Kutoka Ireland Watoa Matibabu Ya Mifupa Kwa Watoto MOI
Habari

Madaktari Kutoka Ireland Watoa Matibabu Ya Mifupa Kwa Watoto MOI

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM: JOPO la madaktari bingwa wa mifupa, ganzi na wauguzi kutoka Ireland limewasili nchini na kuanza kambi maalum ya siku nne ya matibabu ya mifupa kwa watoto katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI).
Kambi hiyo, inayoendeshwa kwa ushirikiano na madaktari wa MOI, inalenga kuwahudumia watoto wenye miguu iliyopinda, miguu mifupi, matege na mivunjiko ya mifupa.
Habari Picha 10076
Akizungumza wakati wa kuwapokea madaktari hao, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Mpoki Ulisubisya, amesema ushirikiano huo na hospitali ya Children’s Health Ireland ya Dublin umeendelea kwa zaidi ya miaka minne, na umechangia kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi.
“Tunashirikiana nao kutoa matibabu ya kibingwa kwa watoto wenye matatizo ya mifupa na pia kujengeana uwezo katika huduma za kibobezi,” amesema Dkt. Mpoki.
Ameongeza kuwa MOI inapanga kuanzisha huduma ya tiba mtandao  ili kuwawezesha wagonjwa kupata matibabu kutoka kwa madaktari bingwa bila kusafiri umbali mrefu.
Kwa upande wake, Dkt. Paula Kelly, bingwa wa mifupa kwa watoto kutoka Ireland, amesema kambi hizo zimekuwa zikisaidia kubadilishana uzoefu na teknolojia za kisasa katika matibabu ya mifupa.
Naye Dkt. Bryson Mcharo, Mkuu wa Kitengo cha Matibabu ya Mifupa kwa Watoto MOI, amesema wagonjwa wote wanapimwa na wale wanaohitaji matibabu zaidi watafanyiwa upasuaji kwa kutumia kifaa maalum cha kisasa cha Taylor Spatial Frame (TSF) kinachotumika kunyoosha miguu na kurekebisha urefu wa mifupa.
Habari Picha 10077

You Might Also Like

Profesa Ndunguru Aongoza Kikao Cha Mawaziri Wa DLCO- EA Akimwakilisha Bashe

Rais Samia kufanya ziara mkoani Morogoro, kuzindua safari za SGR

Majaliwa Aomba Watanzania Wapatiwe Mafunzo Belarus Kuendeleza Kilimo

Mwenyekiti TCCIA Geita Gabriel Ahamasisha Watanzania Kutumia Bidhaa Za Ndani

Wanawake 1,063 Wahitimu Mafunzo Ya Ujuzi VETA Mbeya Kupitia Mpango Wa Rais Samia

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Mwalim: Nikichaguliwa urais, Kigaila atakuwa Waziri Mkuu wangu
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mwalim: Nikichaguliwa urais, Kigaila atakuwa Waziri Mkuu wangu
Habari October 20, 2025
ARTICLE 19,  JOWUTA KUSHIRIKIANA KUIMARISHA HAKI ZA WANAHABARI
Habari October 18, 2025
Mgombea NCCR-Mageuzi Awaasa Watanzania Wasikubali Propaganda
Habari October 17, 2025
Profesa Nombo: Ushirikiano wa VETA, Sekta Binafsi Waimarisha Mafunzo ya Ufundi Stadi
Habari October 17, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?