SERIKALI imeelekeza jumla ya sh bilioni 10 kwa kiwanda Cha kutengeneza viuadudu Cha TBPL kilichoko Kibaha mkoani Pwani kwa ajili ya uendelezwaji na uzalishaji wa dawa na viuatilifu mbalimbali katika mwaka wa fedha 2025/2026.
Mfamasia Mkuu wa Serikali,Daud Masasi amesema hayo mkoani hapa ikiwa ni uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa kiwanda hicho Cha kipekee kwa Afrika na duniani kwa ujumla ambacho kinaendeshwa nna Shirika la Taifa La Maendeleo (NDC).
Akizungumza, Masasi amesema upekee wa kiwanda hicho ndio unaosababisha serikali kuongeza Wigo Wa bajeti kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.
Amesema katika miaka minne ya kipindi Cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, kuanzia 2021/2025 serikali imetoa jumla ya sh bilioni 11.5 ambapo kwa kipindi Cha miaka sita ya mwanzo wakati kiwanda kimeanzishwa fedha zilizotilewa kwa ajili ya kiwanda hicho hazizidi sh bilioni 1.5.
” Ni kiwanda Cha kipekee na serikali inajua umuhimu wake ndio maana kwa bajeti ya mwaka huu zikaelekezwa kiwango hicho Cha fedha ambapo ni sawa na asilimia mia Moja,” amesema Masasi.
Amesema pamoja na kuongeza bajeti katika kiwanda hicho lakini wameanza uhaulishwaji wa utaalam kwa ndani ya nchi, uwekezaji huo ambao unalenga kupunguza kusambaa kwa ugonjwa wa malaria kwa kiwango kikubwa.
Amesema katika mwaka 2014 ugonjwa wa malaria umepungua kutoka asilimia 14 na kufikia asilimia nane kwa sasa na hiyo inatokana na hamasa ya matumizi ya dawa hizo zinazozalishwa na kiwanda hicho kuongezeka.
Kadhalika amesema tayari Halmashauri zote 184 nchini zimepokea dawa hiyo ya viuadudu na kuwataka viongozi husika kuendelea kusimamia.
Akizindua maadhimisho hayo,Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda Na Biashara,Dkt Abdallah Hashil amesema Kwa miaka 10 tangu kuanzishwa kwa kiwanda hicho kimekuwa Cha mfano na chenye kuzalisha dawa za aina mbalimbali zaidi ya tatu
Amesema kwa miaka minne ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, Serikali imepeleka sh bil 11.5 na Kwenye bajeti ya mwaka huu wa fedha 2025/26 kiwanda kimetengewa jumla ya sh bil 10.
“Ni nia ya dhati ya serikali kunyanyua kiwanda hicho,
Dhamira ya kuzalisha dawa ya kuua viuadudu na mpaka sasa Kuna aina tatu za biashara zimeanza kuzalisha…na bidhaa zinazozalishwa hapo hazina kemikali zinaboresha Maisha ya watanzania,” amesema.
Amesema Dawa zinazozalishwa na kiwanda hicho ni za kuuangamiza mazalia ya wadudu Wa malaria na zinauzwa mpaka nje ya mipaka ya Tanzania lengo likiwa ni kuhakikisha Malaria inakwisha nchini.
Amezitaja Nchi ambazo zinasambaziwa dawa hizo kuwa ni pamoja na Uganda, Kenya, Msumbiji, Angola, Niger na kwamba karibu asilimia 25 ya dawa inayozaalishwa inauzwa nje ya NCHI ambayo husaidia pia kupatikana kwa fedha ya kigeni.
Kwa upande wake Mkurugenzi Muendeshaji wa NDC, Dkt Nicholas Shombe amesema hufanya kazi na watalaam kutoka nchinya Cuba na kwamba bidhaa zinazalishwa nchini Tanzania kwa asilimia 100 na watanzania.
Amesema mbali ya dawa ya viuadudu vya malaria pia wanazalsiha bidhaa za mbolea ya kisaikolojia isiyokuwa na kemikali na kwamba ni kiwanda Cha watanzania kwa ajili ya watanzania.