Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM: WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) umeandaa Mkakati wa Usimamizi na Uendelezaji wa Misitu ya Hifadhi ya Mikoko Tanzania Bara
utakaotekelezwa kwa kipindi cha mwaka 2025 hadi 2034, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kulinda mfumo ikolojia wa mikoko.

Ofisa Mratibu wa Mabadiliko ya Tabianchi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Timotheo Mande, amesema mkakati huo ni nyenzo muhimu katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi zinazoathiri maeneo ya mikoko nchini.
“Kwa sasa, mchakato wa kukamilisha mkakati huo unaendelea kwa kukusanya maoni ya wadau kutoka wizara, taasisi za serikali na zisizo za kiserikali pamoja na sekta binafsi,” amesema.

Nayeย Naibu Kamishna wa Uhifadhi TFS, Dkt. Abel Masota, amewataka wadau wote kutoa maoni yao kwa kina na uhuru ili kuhakikisha mkakati unaoandaliwa unakuwa jumuishi na unaotekelezeka kwa ufanisi.Kikao hicho kimeratibiwa kwa ushirikiano na Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira (WWF), ambapo Mwakilishi wa Mkurugenzi wa WWF Tanzania, Yohana Mpagama, ameeleza kuwa shirika hilo litaendelea kushirikiana na serikali katika juhudi za kuhifadhi mikoko nchini.

Mkakati huo unatarajiwa kuimarisha uhifadhi wa mikoko katika eneo la takribani hekta 158,100, linalojumuisha wilaya 14 za ukanda wa pwani. Wilaya hizo ni Mkinga, Tanga na Pangani (Tanga); Bagamoyo, Mkuranga, Mafia na Kibiti (Pwani); Kinondoni, Ilala, Temeke na Kigamboni (Dar es Salaam); Kilwa na Lindi (Lindi); pamoja na Mtwara mjini (Mtwara).

Kikao cha kukusanya maoni hayo kimefanyika leo Aprili 17, 2025, jijini Dar es Salaam kikihusisha jumla ya wadau 75 kutoka maeneo mbalimbali.