MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: 𝐓𝐅𝐒 Y𝐚𝐧𝐝𝐚𝐚 M𝐤𝐚𝐤𝐚𝐭𝐢 W𝐚 M𝐢𝐚𝐤𝐚 1𝟎 Ku𝐞𝐧𝐝𝐞𝐥𝐞𝐳𝐚 N𝐚 K𝐮𝐡𝐢𝐟𝐚𝐝𝐡𝐢 M𝐢𝐬𝐢𝐭𝐮 Ya Mi𝐤𝐨𝐤𝐨 𝐓𝐚𝐧𝐳𝐚𝐧𝐢𝐚 𝐁𝐚𝐫𝐚
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > 𝐓𝐅𝐒 Y𝐚𝐧𝐝𝐚𝐚 M𝐤𝐚𝐤𝐚𝐭𝐢 W𝐚 M𝐢𝐚𝐤𝐚 1𝟎 Ku𝐞𝐧𝐝𝐞𝐥𝐞𝐳𝐚 N𝐚 K𝐮𝐡𝐢𝐟𝐚𝐝𝐡𝐢 M𝐢𝐬𝐢𝐭𝐮 Ya Mi𝐤𝐨𝐤𝐨 𝐓𝐚𝐧𝐳𝐚𝐧𝐢𝐚 𝐁𝐚𝐫𝐚
Habari

𝐓𝐅𝐒 Y𝐚𝐧𝐝𝐚𝐚 M𝐤𝐚𝐤𝐚𝐭𝐢 W𝐚 M𝐢𝐚𝐤𝐚 1𝟎 Ku𝐞𝐧𝐝𝐞𝐥𝐞𝐳𝐚 N𝐚 K𝐮𝐡𝐢𝐟𝐚𝐝𝐡𝐢 M𝐢𝐬𝐢𝐭𝐮 Ya Mi𝐤𝐨𝐤𝐨 𝐓𝐚𝐧𝐳𝐚𝐧𝐢𝐚 𝐁𝐚𝐫𝐚

Author
By Author
Share
2 Min Read

Na Mwandishi Wetu

DAR ES SALAAM: WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) umeandaa Mkakati wa Usimamizi na Uendelezaji wa Misitu ya Hifadhi ya Mikoko Tanzania Bara

utakaotekelezwa kwa kipindi cha mwaka 2025 hadi 2034, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kulinda mfumo ikolojia wa mikoko.

Ofisa Mratibu wa Mabadiliko ya Tabianchi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Timotheo Mande, amesema mkakati huo ni nyenzo muhimu katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi zinazoathiri maeneo ya mikoko nchini.
“Kwa sasa, mchakato wa kukamilisha mkakati huo unaendelea kwa kukusanya maoni ya wadau kutoka wizara, taasisi za serikali na zisizo za kiserikali pamoja na sekta binafsi,” amesema.

Naye  Naibu Kamishna wa Uhifadhi TFS, Dkt. Abel Masota, amewataka wadau wote kutoa maoni yao kwa kina na uhuru ili kuhakikisha mkakati unaoandaliwa unakuwa jumuishi na unaotekelezeka kwa ufanisi.Kikao hicho kimeratibiwa kwa ushirikiano na Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira (WWF), ambapo Mwakilishi wa Mkurugenzi wa WWF Tanzania, Yohana Mpagama, ameeleza kuwa shirika hilo litaendelea kushirikiana na serikali katika juhudi za kuhifadhi mikoko nchini.

Mkakati huo unatarajiwa kuimarisha uhifadhi wa mikoko katika eneo la takribani hekta 158,100, linalojumuisha wilaya 14 za ukanda wa pwani. Wilaya hizo ni Mkinga, Tanga na Pangani (Tanga); Bagamoyo, Mkuranga, Mafia na Kibiti (Pwani); Kinondoni, Ilala, Temeke na Kigamboni (Dar es Salaam); Kilwa na Lindi (Lindi); pamoja na Mtwara mjini (Mtwara).

Kikao cha kukusanya maoni hayo kimefanyika leo Aprili 17, 2025, jijini Dar es Salaam kikihusisha jumla ya wadau 75 kutoka maeneo mbalimbali.

You Might Also Like

Bajeti ya TUGHE 2025 Yaidhinishwa

COSTECH Yasaini Mkataba Ujenzi Jengo La Sayansi, Teknolojia, Ubunifu

TRAWU Yapigania Wafanyakazi TAZARA Nyongeza Ya Mshahara

Ridhiwan Kikwete awasilisha taarifa mwenendo wa ulipaji mafao

REA Yapamba Moto Uhamasishaji Matumizi Ya Umeme

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article COSTECH, CRDB Foundation Yazindua Mikopo Nafuu Kwa Wabunifu
Next Article Simbachawene Asema Serikali Yajivunia Mafanikio TASAF
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Michezo Yapunguza Uhalifu Dodoma
Habari May 25, 2025
Serikali Imetoa Ruzuku Ya Asilimia 20 Hadi 50 Kwenye Mitungi YA Gesi – Kapinga
Habari May 25, 2025
Program Ya Maeneo Yaliyochakaa Nchini Yaandaliwa
Habari May 25, 2025
CCM Kuwezesha Wananchi Kufuatilia Mkutano Mkuu Maeneo Ya Wazi
Habari May 25, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?