Na Mwandishi wetu
DAR ES SALAAM: WAZIRI Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete amekutana na Balozi wa Japan nchini, Yusushi Misawa akiwa ameongozana na ujumbe wake kwa ajili ya kujadili jinsi ya kuwawezesha vijana wa kitanzania.
Ridhiwani amesema pamoja na kuzungumzia mambo mbalimbali katika eneo hilo la vijana wameangalia nafasi za kujifunza kazi na kuimarisha mafunzo ya vijana katika kuongeza ujuzi.


