MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Watumishi Wa Magereza Manyara Wapatiwa Majiko Ya Gesi  
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Watumishi Wa Magereza Manyara Wapatiwa Majiko Ya Gesi  
Habari

Watumishi Wa Magereza Manyara Wapatiwa Majiko Ya Gesi  

Author
By Author
Share
2 Min Read

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imewapatia watumishi wa Jeshi la Magereza mitungi ya gesi na majiko ya gesi ya kupikia ili kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa watumishi na wananchi iliyolenga kufikia malengo yaliyoainishwa kwenye mkakati wa kitaifa wa matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini.

Hayo yamekabidhiwa leo Juni 26, 2025 na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu wakati wa  uzinduzi wa kugawa majiko ya gesi kwa watumishi wa magereza iliyofanyika gereza la Babati mkoani Manyara.

Amesema kuwa, katika mkoa wa Manyara tayari Serikali imegawa mitungi ya gesi na majiko ya gesi yapatayo 330 kwa watumishi wa jeshi la magereza na katika gereza la Babati jumla ya majiko na mitungi 150 wamegawiwa watumishi hao wa magereza.

Amesema kuwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeingia makubaliano na Jeshi la Magereza ya kuwawezesha magereza kuhama kutoka katika matumizi ya nishati isiyo salama kwenda katika matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia katika magereza yote nchini.

“Kuanzia mwanzoni wa mwezi januari 2025 jeshi la magereza walishaingia kwenye matumizi ya nishati safi na salama na tayari wameachana na nishati isiyo salama na chafu kwa afya na mbaya kwa mazingira yetu, ” Ameongeza.

 

 

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA),  Hassan Saidy amewataka watumishi wa jeshi la magereza  kuibeba ajenda ya Rais Samia ya kuwa mabalozi wa nishati safi ya kupikia hapa nchini.

 

Katika hatua nyingine  Saidy ameeleza kuwa, mifumo ya uzalishaji wa bayogesi ipatayo 126 tayari ipo mbioni kuanza kwa kushirikiana na jeshi la magereza ambayo itawezesha ununuzi wa mashine za kutengeneza mkaa mbadala 61, vile vile kuwajengea uwezo watumishi wa jeshi la magereza ya kuendeleza miradi hiyo ya nishati.

 

Kwa upande wake, Mkuu wa Magereza mkoa wa Manyara ACP Solomon Mwambingu amemshukuru Rais Samia kwa kuwapatia watumishi wa magereza majiko ya gesi na mitungi ya gesi na kusisitiza kuwa wataendelea kuwa mabalozi wa nishati safi ya kupikia katika jamii yote inayowazunguka.

You Might Also Like

TPHPA Kuipokea Ndege Yake

‘Skills For Their Future’ Yanufaisha Wanafunzi Zaidi Ya 1000, Walimu 64 

Hospitali ya Temeke kufanyiwa maboresho eneo la huduma Kwa wateja

October 2, 2024

Polisi wazuia uhalifu Tanganyika Packers

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article IITA,TARI, TPHPA Wapambana Kudhibiti Ugonjwa Wa Fungashada Ya Migomba
Next Article Wakulima Wa Zabibu Wakiri Bidhaa Zilizoongezwa Thamani Zina Soko
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Majaliwa Apongeza Jeshi La Magereza Kurasimisha Ujuzi Kwa Wafungwa
Habari August 27, 2025
Mapokezi Ya Katibu Mkuu CCM  Dkt Migiro CCM, Aahidi Ushirikiano
Habari August 27, 2025
Majaliwa Aagiza Kuimarishwa kwa Mafunzo ya Ufundi Stadi Nchini
Habari August 27, 2025
VETA Yaanzisha Kozi Mpya ya Teknolojia ya Mifumo ya Viwandani
Habari August 26, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?