MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Watanzania wasisitizwa kulinda mazingira ya miundombinu ya umeme
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Watanzania wasisitizwa kulinda mazingira ya miundombinu ya umeme
Habari

Watanzania wasisitizwa kulinda mazingira ya miundombinu ya umeme

Penina Malundo
By Penina Malundo
Share
2 Min Read

Na Mwandishi wetu.

Watanzania wameendelea kusisitizwa kutunza mazingira ili kuhakikisha miradi ya kuzalisha umeme kwa njia ya maporomoko ya maji inakuwa endelevu na kuleta tija iliyokusudiwa.

Rai hiyo imetolewa jana Agosti 15 na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB),  Balozi, Meja Jenerali (mstaafu), Jacob Kingu wakati wa ziara ya Bodi hiyo pamoja na Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) walipotembelea miradi ya waendelezaji binafsi wa umeme iliyowezeshwa na REA katika Mkoa wa Njombe.

Wakati wa ziara hiyo, Wajumbe wa Bodi pamoja na Menejimenti waliweza kutembelea mradi wa kuzalisha umeme kwa njia ya maporomoko ya maji wa Lupali uliopo kijiji cha Boimanda Wilaya ya Njombe ambao kukamilika kwake mradi huo utaweza kuzalisha Kilowati 317 (kW) pamoja na mradi wa kuzalisha umeme kwa njia ya maporomoko ya maji wa Lupendo ambao uzalisha Megawati 2.9

“Tumekuwa na muendelezo wa ziara za Bodi pamoja na Menejimenti kutembelea miradi ya waendelezaji binafsi wa umeme katika Mkoa wa Njombe na leo tumetembelea miradi miwili ambayo pamoja na wadau wengine, REA ina mchango mkubwa katika miradi hiyo,”amesema

Amesema serikali kupitia REA imetoa fedha nyingi sana kuwezesha miradi hii kukamilika ili kuendelea kuongeza uhakika wa umeme kwa ajili ya kuwaletea maendeleo mwananchi mmojammoja na Taifa kwa ujumla. Ili miradi hii iwe endelevu tunaendelea kuwasisitiza wananchi kutunza mazingira tuendelee kuwa na maji ya uhakika kuendesha mitambo na hivyo kuwa na umeme wa uhakika pia,” amesisitiza Mwenyekiti Kingu.

Kwa upande wake msimamizi wa mradi wa Lupali ambao unaendeshwa na shirika la Benedictine Sisters of St. Gertrud Convent Imiliwaha, Sister Imakulata Mlowe ameishukuru REA kwa ufadhili walioutoa kuwezesha mradi huo ambapo REA imechangia asilimia 77 ya gharama za ujenzi wa mradi huo ambao unagharimu Zaidi ya Shilingi Bilioni 6.

Naye Meneja Mkuu na Mkurugenzi wa Rift Valley Energy, Deo Massawe amesema kuwa tangu kuanza kwa mradi wa kuzalisha umeme kwa njia ya maporomoko ya maji wa Luponde wameweza kuunganisha wananchi, shule, hospitali pamoja na viwanda vya chai.

You Might Also Like

TPDC  Yaibuka Mshindi Sabasaba Yapata Tuzo Ya Tano

Usajili Kwa Njia Ya Mtandao, Umeharakisha Ufunguaji Mashauri

Mbunifu Alilia Uwepo Wa Miongozo Kwa Wagunduzi

Jaffo Aagiza Kufufuliwa Vilivyokuwa Viwanda Vya Serikali

Tigo yawafikia wakulima, wafugaji. Wavuvi nanenane Dodoma

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Rais Samia awasili Zimbabwe
Next Article Changamoto uchakataji Mkonge kupatiwa ufumbuzi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vyombo vya Habari ni Kama Maji’ -Biteko 
Habari July 10, 2025
TARI Kihinga Yainua Kilimo Cha Michikichi Kigoma
Habari July 10, 2025
Mchengerwa Apongeza Shule Ya Sekondari Kibaha Kwa Ufaulu Wa Hali Ya Juu
Habari July 9, 2025
NIT Yasema Ina Uwezo Wa Kufundisha Kozi Ya Urubani
Habari July 9, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?