MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Wananchi Waendelee Kupewe Elimu Kuhusu Bioteknolojia
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Wananchi Waendelee Kupewe Elimu Kuhusu Bioteknolojia
Habari

Wananchi Waendelee Kupewe Elimu Kuhusu Bioteknolojia

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read

Na Lucy Ngowi

DAR ES SALAAM:WANANCHI wanapaswa kuelimishwa na kuelewa sera, sheria, mifumo, kanuni na miongozo inayosimamia matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa ili kuondoa hofu na dhana potofu kuhusu teknolojia hiyo miongoni mwa baadhi ya watu.

Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Toba Nguvila amesema hayo katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Bioteknolojia Tanzania (BST),alipomwakilisha Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa RAIS, Cyprian Luhemeja.

Nguvila amesema utoaji elimu huo ni jukumu la kila mmoja ikiwemo serikali na asasi mbalimbali ikiwemo BST.

‘’Ninaamini kuwa ushirikiano miongoni mwetu ni moja ya nyenzo muhimu katika kufanikisha matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa kwa maendeleo ya nchi yetu.

‘’Kwa hiyo tunatarajia kupata ushirikiano timilifu na endelevu kutoka kwenu katika kuelimisha wananchi dhana nzima ya bioteknolojia kwa kukuza uelewa kwa jamii kuhusu faida za bioteknolojia hasa katika sekta ya kilimo,”amesema.

Amesema anaelewa kwamba BST kimekuwa kinaendesha semina na mashauriano mbalimbali ya kukuza uelewa na ufahamu wa wadau wengine kwa kuchangia katika kukuza uelewa wa jamii kuhusu teknolojia hiyo.

Amewataja wadau hao kuwa ni pamoja Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, vyuo vikuu, vituo vya utafiti nchini, vyombo mbalimbali vya habari,  program ya Jukwaa la Biotekinolojia (OFAB)Tanzania na Shirika la Kimataifa linalohusika na Biotknolojia ya Kilimo kwa kujihusisha na uhandisi wa vinasaba (ISAAA)

Pia amesema pamoja na vyuo kujenga uwezo wa rasilimali watu wa kuendeleza tasnia ya bioteknolojia, wahitimu wa kozi hiyo wanakosa ajira hivyo amelichukua kwa ajili ya kulifikisha wizara husika ili liweze kupatiwa ufumbuzi.

Amesema itakuwa haina maana yoyote kwa vyuo kuendeleza kuzalisha wataalam wa tasnia hiyo muhimu halafu wanashindwa kuingia katika soko la ajira.

Naye Mwenyekiti wa BST, Profesa Peter Msolla amesema kwa mwaka 2024 taasisi hiyo imeendelea kuchangia utekelezaji wa sera ya Mazingira ya mwaka 2021 iliyozinduliwa na Makamu wa Rais Philip Mpango Februari 12, 2022.

‘’Asasi yetu inazingatia maelekezo ya kisera yanayolenga, pamoja na mambo mengine katika uhifahi wa mazingira, kujenga uwezo na uelewa katika usimamizi na matumizi salama ya biotknolojia ya kisasa,’’amesema.

Amesema serikali imejikita katika ujenzi wa uchumi wa viwanda ili kuchochea mageuzi makubwa ya kiuchumi na maendeleo ya watu kwa kurejea dira ya Maendeleo ya watu kwa kurejea dira ya taifa na kuandaa muendelezo wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025.

 

You Might Also Like

Tanzania, Japan Kushirikiana Ukuzaji Ujuzi Kwa Vijana

Manara: Sitapambana na Wafanyabiashara, Nitawatetea

VETA Kujenga Mahusiano Na Wenye Ujuzi, Wabunifu

Sheria ya ajira, mahusiano kazini ipitiwe upya

Kamati Ya Bunge Ya Ustawi Na Maendeleo ya Jamii, Yaipongeza Serikali Uwekezaji Kiwanda Cha Chai

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Kampuni ya Kichina CCCC yatoa msaada wa vitabu UDSM
Next Article Kilimo Shadidi Kinapunguza Uzalishaji Wa Gesi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?