MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Wananchi Wahimizwa Kulinda Maeneo Yaliyohifadhiwa  Kisheria- Kamishna  Wakulyamba
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Wananchi Wahimizwa Kulinda Maeneo Yaliyohifadhiwa  Kisheria- Kamishna  Wakulyamba
Habari

Wananchi Wahimizwa Kulinda Maeneo Yaliyohifadhiwa  Kisheria- Kamishna  Wakulyamba

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Mwandishi Wetu  Butuli Simiyu
WIZARA ya Maliasili na Utalii imetoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kulinda maeneo yanayohifadhiwa kisheria na ku kudhibiti  Wanyamapori .
Imesema udhibiti huo ni pamoja na  wananchi kuacha kuvamia na kulima mazao yanayopendwa  na wanyamapori hususan tembo pamoja na kuchunga mifugo maeneo ya wanyama hao.
Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba alipotembelea  Kijiji cha Butuli kinachopakana na  Pori la Akiba Maswa.
Aidha ameshuhudia namna baadhi ya wananchi wakiendesha shughuli za kibinadamu pembezoni mwa mpaka na wengine ndani ya eneo lililohifadhiwa kisheria.
Akiongea na maofisa na askari wa Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA), Wakulyamba amesema kuwa  Waziri Balozi Dkt  Pindi Chana ameagiza jitihada zaidi ziongezwe katika kuhakikisha wananchi wanakuwa salama pamoja na mali zao na hasa kudhibiti vifo vinavyotokana na tembo.
 Wakulyamba ameongeza kuwa Waziri Balozi Dkt. Chana ameagiza kuendelea kujenga mahusiano mema na wananchi wanaozunguka maeneo yaliyohifadhiwa kwa kuhakikisha wanapatiwa elimu ya kutosha, pamoja na kuwashirikisha kikamilifu katika mapambano dhidi ya wanyama hao.
 “Sisi wahifadhi tunayafahamu kitaaluma maeneo tunayoyalinda kwa kuwa tumesomea na tumeletwa hapa kufanya kazi lakini wananchi wanaoyazunguka maeneo ya Hifadhi wao wanayafahamu kwa asili, wamezaliwa hapo, wanaishi hapo hivyo wanayajua kwa undani mkubwa. Tukishirikiana nao watatusaidia hata kuwajua wahalifu dhidi ya maliasili zetu”, Amesema  Wakulyamba.
Aidha, Kamishna  Wakulyamba amewataka askari hao wa TAWA kuzingatia mafunzo waliyopewa na Maofisa wa Polisi Mrakibu wa Polisi Joseph Jingu na Mrakibu wa Polisi Ocsar Felician pamoja na Ofisa Mhifadhi Edwin Nyerembe kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii juu ya Haki za Binadamu na Utawala wa Sheria.
Mafunzo hayo ni utekelezaji wa Maelekezo ya Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassan  yaliyotokana na maoni ya Tume ya Jinai.
Mafunzo mengine yanayotolewa na Maofisa hao ni pamoja na matumizi sahihi na salama ya Silaha  yakilenga kuboresha utendaji kazi ndani ya Jeshi hilo la Uhifadhi.
Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli Katika Pori la Akiba Maswa,  Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi  Saidi Kabanda, ambaye ni  Kaimu Kamanda wa Uhifadhi Kanda ya Ziwa TAWA, amesema moja ya jitihada zilizochukuliwa  katika Mkoa wa Simiyu ni pamoja na kujengwa kwa vituo vinne vya kudhibiti Wanyamapori wakali na waharibifu, kukarabari vituo vingine vinne pamoja na kuongeza askari wa Uhifadhi na wa Vijiji (VGS).
Naye Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Butuli Emmanuel Fabian Machibya ameipongeza Serikali ya awamu ya sita kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kwa hatua zinazochukuwa za kushirikiana na wananchi wa kijiji cha Butuli  katika mapambano dhidi ya Wanyamapori wakali na waharibifu hali inayoleta faraja zaidi kwa wananchi.

You Might Also Like

Jeshi La Uhifadhi Wasisitizwa Kuzingatia Misingi ya Haki za Binadamu

Elimu Itolewe Kuhusu Ufahamu Wa Kuwepo Kwa Fedha Maalum – Ridhiwani

Mtoto Wa Miaka Sita Ashinda Ashindano Ya Kuhifadhi Quraan Mkoa Arusha

Ridhiwan Kikwete aitaka LESCO kushirikiana na serikali

Wajadili uendelezaji mazao ya utalii

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Polisi Yaimarisha Usalama Timu za Simba na Yanga Kesho
Next Article Kamati Ya Bunge  Yaridhishwa Na Ujenzi Wa Jengo La Kituo Cha Zimamoto, Mtumba
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?