Na Mwandishi Wetu
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio ameongoza kikao cha Tatu cha Kamati ya Uongozi ya Mradi wa usafirishaji umeme wa msongo wa kilovoti 400 wa Tanzania- Zambia (TAZA) .
Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Nishati Dar es Salaam.
Aidha wajumbe wa kikao hicho wamejadili utekelezaji wa mradi hadi kufikia Julai, 2025 kimewataka wakandarasi wote wanaotekeleza mradi huo kukamilisha kazi mapema kwa mujibu wa mkataba.
Mradi mkubwa wa usafirishaji umeme wa TAZA unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kilovoti 400 kutoka Iringa hadi Sumbawanga na kuunganisha Tanzania na Zambia.
Pia miradi unahusisha ujenzi wa vituo vya kupoza umeme vya Iringa, Mbeya, Tunduma na Sumbawanga pamona na mfumo wa kutoa huduma ambao utawezesha kuunganisha Bara la Afrika kwa nishati ya umeme kutoka Afrika Kusini hadi Ethiopia.
Kikao hicho kimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Wizara ya Nishati na taasisi zake pamoja na Wizara ya Fedha.