MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Wahamasika Kutumia Mbegu Bora Za Karanga Zilizofanyiwa Utafiti Na TARI
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Wahamasika Kutumia Mbegu Bora Za Karanga Zilizofanyiwa Utafiti Na TARI
Habari

Wahamasika Kutumia Mbegu Bora Za Karanga Zilizofanyiwa Utafiti Na TARI

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Lucy Ngowi
MANYARA: WAKULIMA wa zao la Karanga wapo tayari kutumia mbegu bora za Karanga zilizofanyiwa utafiti kwa kuwa zina tija kubwa ikilinganishwa na mbegu za kienyeji ambazo wamekuwa wakitumia.
Utayari wa wakulima hao kutoka Kijiji cha Kiru six, Kata ya Kiru Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara umeonekana katika siku ya Mkulima wa Karanga iliyofanyika Kijijini hapo ikiratibiwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) kupitia kituo cha TARI Naliendele.
Mkulima Halima Nada ameitaja mbegu iliyofanyiwa utafiti ya TARIKA1, kuwa inamfaa zaidi kutokana na alivyoiona imefanya vizuri kwenye shamba darasa lililowekwa Kijijini hapo kwa kuwa ni tofauti na mbegu alizozizoea.
Amesema utofauti aliouona ni mbegu hiyo kutoshambuliwa na magonjwa, ina ladha tamu pia inawahi kukomaa huku tija ikiwa kubwa.
“Hii Mbegu ya TARIKA1 imechelewa kupandwa kulinganisha na hizi Mbegu zetu za kienyeji lakini imewai kukomaa na imezaa zaidi ya hizi Mbegu zetu hivyo binafsi msimu ujao nitalima zaidi hii mbegu ambayo pia inaonesha haishambuliwi na magonjwa,” amesema.
Pia Mkulima na Mwenyekiti wa Baraza la Wakulima Tanzania,  Jitu Vrajilal  Son,   amesema mbegu za karanga zilizofanyiwa Utafiti zina tija katika mnyororo mzima wa thamani kwa kuwa zinajibu mahitaji ya wadau kama vile upatikanaji wa karanga za kwa ajili ya Siagi.
Mkulima JituSon, ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Babati amesema alipata mafunzo  ya uzalishaji Mbegu kutoka Taasisi ya Uthibiti Ubora wa Mbegu (TOSCI)  hivyo  kutokana na ubora wa mbegu za TARI na  mwitikio mzuri wa wakulima  ataanza kuzalisha mbegu hizo kwa wingi ili kukidhi hitajio la Wakulima ambao wameeleza utayari kuzitumia.
Naye Mtafiti wa zao la Karanga kutoka TARI Naliendele, Anthony Bujiku amesema lengo lao kufika Kijiji hapo ni kufanya siku ya Mkulima wa Karanga ambapo wamefundisha kanuni bora za kilimo cha zao hilo ikiwa ni pamoja na utambuzi na Uthibiti wa visumbufu katika zao la Karanga.
Mtafiti Bujiku amewashauri wakulima kuzingatia matumizi ya mbegu bora pamoja na kufuata kanuni bora ili kujiongezea tija.
Pia ametoa wito kwa wakulima kushirikiana na Maofisa Ugani walioko katika maeneo yao  ili kupata msaada wa kitaalamu katika mambo mbalimbali ya kilimo ili waweze kuongeza tija.

You Might Also Like

Watumishi wa serikali watakiwa kutokuwa kikwazo kwa wawekezaji

Nchimbi Agongelea Nyundo Kwa Wagombea Watoa Rushwa

Makalla Aeleza Jinsi CCM Ilivyosimamisha Nchi Mchakato Kura Za Maoni

Masoko mapya nje ya nchi kuipatia nchi sh. trilioni 10

Aprili 2025 Matokeo Awamu Ya Kwanza, Maoni Dira Ya Taifa Na Maendeleo 2050 Kutolewa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Mdemu Awataka Wafanyabiashara Ndogo Ndogo Kuchangamkia Mkopo
Next Article Ripoti Ya Bodadoda Yazinduliwa
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?