Na Lucy Lyatuu
SHRIKA la CVM kwa kushirikiana na Mamlaka Ya Ufundi Stad nchini (VETA) kwa ufadhili wa Serikali Ya Italy wametoa mafunzo kwa wafanyakazi wa maju mbani wapatao 700 tangu kuanza kwa mtaala wa wafanyakazi wa majumbani uliozinduliwa April ,mwaka jana .
Mtaalam wa masuala ya jinsia Maria Shimba amesema hayo wakati akizungumza na gazeti la MFANYAKAZI katika banda la VETA kwenye maonesho ya 49 ya biashara ya kimataifa maarufu kama sabasaba yanayoendelea Dar es Salaam.
Amesema wafanyakazi hao tayari wamesoma masomo mbalimbali ikiwemo namna ya kuandaa chakula namna ya kuwajali watoto na wazee na wa Sasa wako kwa waajiri wao.
Ameyataja masomo mengine waliyosoma kuwa ni pamoja na ujuzi wa kimaisha,usalama jikoni,usafi,uvumilivu,huduma kwa wateja pamoja na haki za kazi.
Amesema kupitia maonesho hayo wako katika maonesho hayo kwa ajili ya kuhamasisha kuhusu mtaala huo kwa watanzania ili kujua kuwa zipo kozi mbalimbali zinazotolewa kwa wafanyakazi wa majumbani ikiwemo ya mwezi mmoja,mitatu hadi sita.
Amesema mafunzo hayo yanatolewa katika vyuo sita vya VETA vya Tanzania Bara na Zanzibar ikiwemo vyuo vya Chang’ombe, Dodoma,Lindi,Tanga,Iringa na Mikumi.
Amesema kwa upande wa Zanzibar mafunzo yanatolewa katika chuo cha VETA cha Mkokotoni,Makindudi na Daya Pemba na mwanafunzi akihitimu anapewa cheti cha ubobezi wa kazi za majumbani.
Maria amesema wanatumia maonesho ya sabasaba kuelezea kuhusu mtaala huo i ambao ni msaada wa kupunguza madhila kwa wafanyakazi wa majumbani pamoja na kupokea ujuzi.