Na Danson Kaijage
DODOMA: MAMLAKA ya Mkemia Mkuu wa Serikali, imepokea majarida jinai ya kupima vinasaba 524 kwa mwaka mmoja, ambayo kipimo kimoja kinagharimu Sh laki moja.
Akitoa taarifa ya mafanikio kwa miaka minne ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan. Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fedelice Mafumiko amesema ufunguaji wa majarida jinai hayo, inaonesha ni namna gani wananchi wamekuwa na uelewa wa kupima vinasaba.

Pia amesema mamlaka hiyo imepata wito wa kusaidia kutoa ushahidi wa kimahakama 6986.
Amesema mafanikio hayo yanatoka na utendaji kazi wa ushirikiano na watendaji wa Mamlaka husika katika kufikia lengo la utoaji huduma bora kwa jamii.

Ndani ya miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita,
Mamlaka hiyo mefanikiwa kujenga jengo la makao Makuu lililopo Jijini Dodoma na hadi kukamilika kweke limegharimu Sh. Bilioni 8.14
Pia amesema kuwa Mamlaka imefanikiwa kujenga maabara za kikanda na kujenga nyumba za watumishi mipakani.