Na Lucy Lyatuu
BARAZA la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) limebainisha mazao ya parachichi, kakao, kahawa, mafuta
mazao ya kilimo cha bustani, ngozi, na viungo, kuwa ni moja ya bidhaa muhimu zinazoweza kuongeza ufanyaji biashara ndani ya soko Huru la Afrika (AfCTA).
Meneja Biashara ya Bidhaa kutoka EABC Frank Daffa amesema hayo leo Dar es Salaam Kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa EABC,Adria Njau katika ufunguzi wa mafunzo kwa vijana namna ya kushiriki katika soko la AfCTA.
Amesema mpango huo wa mafunzo ni sehemu ya ushirikiano mpana kati ya EABC na Kituo Cha Kitaifa Cha Biashara (ITC) ili kuboresha ufikiaji wa soko na
ushindani kwa zaidi ya wajasiriamali vijana milioni 400 (MSMEs,) wanawake, na vijana katika minyororo ya thamani ya kikanda.
“Kwa pamoja, tunalenga kujenga ujuzi na uwezo wa
wajasiriamali, kuwawezesha kustawi chini ya soko la
Eneo Huru la Biashara la Bara (AfCFTA),” amesema na kuhimiza vijana kuchangamkia soko hilo.
Amesema mafunzo hayo yanasaidia kuwa na mfumo wa ubora wa biashara wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) .
Amesema mafunzo yanalenga kuwawezesha vijana kuwa na maarifa na ujuzi wa namna ya kufanya biashara chini ya soko la AfCFTA.
Amesema pamoja na kuanza kwa biashara isiyo na ushuru chini ya AfCFTA Januari 2021, kuna haja ya kuunda upya mazingira ya biashara ya Afrika.
Njau amesema kwa mujibu wa takwimu za kibenki inaelezwa kuwa utekelezaji kamili wa AfCFTA unaweza kuimarisha mapato ya kikanda kwa dola bilioni 450 na kuinua watu milioni 30 kutoka katika umaskini uliokithiri ifikapo 2035.
Hata hivyo, amesema ni lazima kushughulikia vikwazo virokanavyo na uwezo mdogo wa kufanya biashara Kwa vijana.
Amesema Vijana milioni 400 wa Afrika ndio uti wa mgongo wa uchumi na ufunguo wa kufungua uwezo kamili wa AfCFTA.
Kwa upande wake Mwakilishi kutoka ITC, Richard Adu Gyamfi amesemaafunzo Kwa vijana yanasaidia kuwa washindani katika soko na kufahamu bidhaa zilizopo kwenye minyororo wa uhitaji.
” Umuhimu wa mafunzo ni kuwezesha vijana kulijua soko,bidhaa zinazotakiwa na ubora wake lakini pia kuwa na taarifa kamili namna ya kufikia huko,” amesema