MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: VETA Yajipanga Kutoa Mafunzo Yanayoendana na Teknolojia ya Kisasa
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > VETA Yajipanga Kutoa Mafunzo Yanayoendana na Teknolojia ya Kisasa
Habari

VETA Yajipanga Kutoa Mafunzo Yanayoendana na Teknolojia ya Kisasa

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
MBEYA: MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Anthony Kasore, amesema VETA imejipanga kuhakikisha Watanzania wanapata ujuzi unaokidhi mahitaji ya soko la ajira la kisasa kwa kutumia teknolojia za kisasa.
Akizungumza alipotembelea Chuo cha VETA Mkoa wa Mbeya, Kasore amesema taasisi hiyo inaendelea kuboresha karakana na vifaa vya kufundishia ili kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia, hususan katika fani kama umeme wa magari, useremala, ushonaji wa mabomba, urembo na ususi.
“Dunia ya leo inahitaji mafundi wanaotumia teknolojia kugundua matatizo, si kusikiliza sauti ya gari. Mafunzo yetu sasa yanazingatia hilo,” amesema.
Kasore ametaja pia kuwa VETA imeanza kutoa mafunzo ya sanaa za maonyesho kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa Tanzania  (BASATA) na Bodi ya Filamu, ili kukuza vipaji katika uandaaji wa video, muziki na tamthilia.
“Ujuzi si lazima uwe kiwandani. Hata sanaa ni eneo la ajira na kipato, na VETA tunalipa uzito huo,” amesema.
Kwa upande wa watu wenye mahitaji maalum na wanaoishi mazingira magumu, Kasore amesema VETA hutoa mafunzo kwa zaidi ya watu 1,000 kila mwaka kupitia miradi maalum na ina miundombinu rafiki kwa makundi hayo.
Aidha, ameeleza kuwa ujenzi wa vyuo vipya 65 unaoendelea nchini kote ni sehemu ya mpango wa serikali kufikisha elimu ya ufundi karibu zaidi na wananchi, kwa kuzingatia mahitaji ya kiuchumi ya kila eneo.
Kasore pia amebainisha kuwa Oktoba 17, VETA itakutana na waajiri na wadau wa viwanda kwa lengo la kuboresha mitaala na kuimarisha ubora wa mafunzo.
“Ushirikiano na waajiri unahakikisha tunazalisha wahitimu wenye ujuzi unaohitajika kazini,” alisema.
Kwa ujumla, Kasore amesisitiza kuwa dhamira ya VETA ni kumwezesha kila Mtanzania kupata ujuzi utakaomsaidia kuajiriwa, kujiajiri au kuajiri wengine – ikiwa ni mchango muhimu kuelekea Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050.

You Might Also Like

Si ruhusa kufuga, kuchunga, kuvua maeneo ya umwagiliaji

Washauri Serikali Kutumia Fedha Za Miradi

Halmashauri Zahimizwa Kujenga Viwanda Vya Michezo.

Watumishi Wa Afya Waliofadhiliwa Watakiwa Kukamilisha Taratibu Ifikapo Novemba 22,2025

TARI Yanufaisha Wadau Wa Kilimo, Ugunduzi Wa Mbegu Bora Na Za Kisas

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar Atoa Rai Kuhusu Afya ya Akili kwa Vijana
Next Article Elimu ya Ufundi Yachangia Maendeleo ya Taifa – VETA
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Msama Aipongeza Hotuba Ya Samia, Atoa Neno Kwa Vijana, Wazee, Wanaharakati
Habari December 4, 2025
Profesa Silayo Aaga, Jawara Kuchukua Uongozi Mpya wa AFWC25
Habari December 3, 2025
Mpango Wa Taifa Wa Teknolojia Uko Mbioni Kuja-Serikali
Habari December 3, 2025
Petroli Yaendelea Kushuka Bei Desemba
Habari December 3, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?