MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Usekelege: Kati ya Migogoro Tunayoipokea Ipo ya Wafanyakazi Majumbani
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Usekelege: Kati ya Migogoro Tunayoipokea Ipo ya Wafanyakazi Majumbani
Habari

Usekelege: Kati ya Migogoro Tunayoipokea Ipo ya Wafanyakazi Majumbani

Author
By Author
Share
2 Min Read

Na Lucy Ngowi

MKURUGENZI waTume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) Usekelege Mpulla amesema kati ya migogoro inayopokelewa miongoni mwao ipo ya wafanyakazi wa majumbani, huisikiliza na kuitendea haki.

Amesema hayo alipozungumza na MFANYAKAZI kuhusu tume hiyo endapo kama imekuwa ikipokea migogoro ya wafanyakazi hao kwa ajili ya kusikiliza ili sheria iweze kuchukua hatua.

Mpulla amesema, “Tunapozungumzia Hakikazi Tanzania hakuna mfanyakazi aliyebaguliwa. Haijalishi mfanyakazi ni wa kada gani kwani sheria imempa haki zote,”.

Pia amesema anapozungumziwa mfanyakazi wa ndani sheria iliyopo haijamtenga, “Tunapozungumzia haki, maslahi, mgogoro wa kikazi bado ana haki,”.

“CMA haijawatenga wafanyakazi wa ndani, tunatoa wito wafahamu haki zao zimelindwa kisheria. CMA inafungua milango kwa wafanyakazi hao endapo wakiachishwa kazi, wakilipwa kima cha chini, pia wasipolipwa,” amesema.

Ameongeza kuwa hivi karibuni wamekuwa wakizungumzia mfumo wa utatuzi wa migogoro na usajili wa migogoro, hivyo mfanyakazi aliyeona vigumu kufikia tume, atajisajili mgogoro wake kupitia mfumo huo.

Amesema mfumo huo ukitumika mfanyakazi atakayekuwa ameona vigumu kufika kwenye tume hiyo ataweza kujisajili kupitia mfumo.

Amesema katika Sheria za Kimataifa zinazosimamiwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO), kuna mkataba namba 189 umebainisha hizo haki kwamba wafanyakazi wa majumbani wapewe mikataba.

“Hivi sasa tunafanyakazi kwa karibu na ILO. Kuna Mradi unakuja kutakuwa na mpango mkubwa wa kuwafikia wafanyakazi wa ndani na haki zao zinafikiwa,” amesema.

Pia amewataka wafanyakazi hao kutokusita kufika CMA endapo wanaona hawajatendewa haki na waajiri wao.

 

You Might Also Like

Zitumieni fursa za misitu na nyuki-Tafori

Wakulima wafunzwa kuhusu mlipuko wa panya TPHPA

Dhibitini Magonjwa ya Mlipuko-Mchengerwa

UDSM Yaanzisha Mkakati Kuokoa Nyuki Wadogo

Watakiwa kufanya utafiti kubaini chanzo cha makosa ya walimu

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TEA, TotalEnergies Marketing Ltd Wakabidhi Madawati 130 Wilayani Kibiti
Next Article Ujenzi wa Majengo Mapya 67 Ya Halmashauri Yamekamilika-Mchengerwa
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Tulia Atoa Taarifa Kifo Cha Ndugai
Habari August 6, 2025
Tume ya Kurekebisha Sheria Yaelimisha Umma Kuhusu Haki za Wanyama
Habari August 6, 2025
Bundi Wasaidia Kupambana na Panya: Teknolojia Asilia Inayobadili Maisha ya Wakulima
Habari August 6, 2025
Ofisa wa TARI Kuwapo Kila Kituo cha Umwagiliaji – Naibu Katibu Mkuu
Habari August 6, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?