Na Lucy Lyatuu
SERIKALI imesema ukatili wa kijinsia unaendelea kuwa moja ya changamoto kubwa za haki za binadamu nchini, huku takwimu za kitaifa zikionesha kuwa asilimia 39.5 ya wanawake wenye umri kati ya miaka 15 hadi 49 wamewahi kukumbwa na ukatili wa aina mbalimbali ikiwemo wa kimwili, kihisia na kingono kutoka kwa wenza wao.
Aidha wadau wameshauri kuimarisha Kwa usalama wa kidigitali na kushuhulikia ukatili wa kijinsia kupitia teknolojia ( TFGBV) Ili kuruhusu wanawake na wasichana kushiriki kikamilifu katika elimu,fursa za kiuchumi,uongozi ma Maisha ya kiraia.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watu wenye Ulemavu Zanzibar, Abeda Rashid Abdallah amesema hayo Dar es Salaam wakati akizungumza katika mkutano wa kitaifa kuhusu viashiria vya ukatili wa kijinsia vinavyofanyika kupitia teknolojia (TFGBV).

Mkutano huo umeandaliwa na Shirika la kimataifa linaloshughulika na idadi ya watu (UNFPA )kwa kushirikiana na Shirika la C-Sema, ukilenga kuimarisha hatua za Tanzania katika kukabiliana na ongezeko la ukatili wa kidijitali dhidi ya wanawake na watoto.
Akifafanua zaidi, Abeda amesema kuwa ukatili wa kijinsia unaowezeshwa na teknolojia ni tatizo linalokua kwa kasi, likijumuisha vitendo kama usambazaji wa picha za faragha bila ridhaa, unyanyasaji wa kingono mtandaoni, vitisho vya kidijitali, lugha za chuki na matusi.

Amesisitiza kuwa vitendo hivyo vinaathiri kwa kiasi kikubwa ustawi wa kisaikolojia na kijamii wa waathirika, hususan wanawake na wasichana.
Aidha, ameongeza kuwa zaidi ya nusu ya wanawake vijana wamewahi kukumbana na unyanyasaji mtandaoni, hali inayotia wasiwasi mkubwa katika kipindi hiki ambacho matumizi ya teknolojia yanaongezeka kwa kasi nchini.
Mwakilishi Mkazi wa UNFPA nchini Tanzania, Melissa Barrett ameeleza kuwa teknolojia inapaswa kuwa chombo cha kuwawezesha watu badala ya kuwa jukwaa la kuumiza huku akisisitiza kuwa kadri upatikanaji wa intaneti unavyozidi kuongezeka, ni lazima kuwepo na hatua madhubuti za kuhakikisha wanawake na wasichana wanatumia nafasi za kidijitali kwa usalama bila hofu ya kunyanyaswa.
“Ni muhimu ubunifu wa Kidigitali kuchangia usawa wa kijinsia na ulinzi wa haki za binadamu,”amesema Mellissa.
Kwa upande wake, Balozi wa Finland nchini Tanzania, Theresa Zitting amesema kupitia ushirikiano uliopo kati ya serikali ya Finland, UNFPA na serikali ya Tanzania, wamejizatiti kushiriki utaalamu wa kimataifa katika maeneo ya utawala wa kidijitali, usalama wa mtandao na matumizi ya teknolojia yenye kuzingatia maadili ambapo juhudi hizo zinalenga kuhakikisha maendeleo ya teknolojia yanachangia kukuza usawa wa kijinsia badala ya kuongeza pengo la ukatili.
Kwa upande wake Ofisa program za jinsia kutoka UNFPA Ally Ahmad amesema mkutano huo una umuhimu mkubwa katika kuleta uelewa wa pamoja kuhusu changamoto ya udhalilishaji wa kijinsia unaochochewa na matumizi ya teknolojia nchini Tanzania.
Kupitia majadiliano ya wadau mbalimbali, ikiwemo serikali, taasisi za kimataifa kama UNFPA, wataalamu wa teknolojia na wanajamii

