Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: JUMLA ya watahiniwa wa Shule 477,262 kati ya 516,695 wenye matokeo ambao ni sawa na asilimia 92.37 wamefaulu kwa kupata Madaraja ya I, II, III na IV.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania, Dkt. Said Mohamed amesema hayo wakati akitoa taarifa ya matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana 2024.
Dkt. Mohamed amesema mwaka juzi 2023 watahiniwa
waliofaulu walikuwa 471,427 sawa na asilimia 89.36. Hivyo, ufaulu umeongezeka kwa asilimia 3.01.
“Kati ya watahiniwa 477,262 waliofaulu, Wasichana ni 249,078 sawa na asilimia 91.72 ya Wasichana wote wenye matokeo na Wavulana ni 228,184 sawa na asilimia 93.08 ya Wavulana wote wenye matokeo,” amesema.
Kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea amesema, waliofaulu mtihani ni 15,703 sawa na asilimia 62.51.
“Mwaka 2023 Watahiniwa wa Kujitegemea 13,396
sawa na asilimia 52.44 walifaulu mtihani huo. Hivyo, ufaulu wa Watahiniwa wa Kujitegemea umepanda kwa asilimia 10.07 ikilinganishwa na mwaka 2023,” amesema.
Kuhusu usajili amesema Jumla ya watahiniwa 557,796 walisajiliwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne wakiwemo Wasichana 296,051 ambao ni asilimia 53.08 na Wavulana 261,745 sawa na asilimia 46.92.
“Kati ya watahiniwa 557,796 waliosajiliwa, watahiniwa
wa Shule walikuwa 529,329 na watahiniwa wa Kujitegemea walikuwa 28,467,” amesema.
Amesema kati ya watahiniwa 529,329 wa Shule waliosajiliwa, watahiniwa 517,460 sawa na asilimia 97.76 walifanya mtihani ambapo Wasichana walikuwa
271,918 sawa na asilimia 97.54 ya Wasichana wote huku Wavulana wakiwa 245,542 sawa na asilimia 98.00.
271,918 sawa na asilimia 97.54 ya Wasichana wote huku Wavulana wakiwa 245,542 sawa na asilimia 98.00.
Amesema watahiniwa 11,869 sawa na asilimia 2.24 hawakufanya Mtihani.
Kati ya watahiniwa 28,467 wa Kujitegemea waliosajiliwa,amesema watahiniwa 25,151 sawa na asilimia 88.35 walifanya Mtihani na watahiniwa 3,316
sawa na asilimia 11.65 hawakufanya Mtihani.
sawa na asilimia 11.65 hawakufanya Mtihani.