Na Lucy Lyatuu
CHUO Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) kwa kushirikiana na Watumishi Housing Investment (WHI),wamesaini mkataba wa makubaliano wa ujenzi na uendeshaji wa Kituo Cha kisasa Cha Biashara chuoni hapo kitakachogharimu ujumla ya sh bilioni 8.3.
kitakachotoa huduma mbalimbali kwa wananchi, wanafunzi na wafanyakazi kwa ujumla.
Mradi huo utafanyika ndani ya Chuo katika eneo lenye ukubwa Wa Mita za mraba 12498.5 na ujenzi utakamilika ndani ya miezi 18 kuanzia sasa.
Akizungumza wakati Wa utiaji Saini mkataba huo kwenye hafla iliyofanyika UDSM, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Profesa William Anangisye amesema baada ya kukamilika utaendeshwa na WHI kwa miaka 15
Amesema baada ya kipindi hicho Cha uendeshaji ,kituo kitakabidhiwa kwa UDSM ambapo wataamua kuendeshwa wenyewe au kuweka mtu mwingine.
Amesema Kituo hicho kitakuwa na ujenzi Wa majengo ambayo yatajumuisha ofisi mbalimbali, maduka makubwa, na maeneo ya michezo ya watoto , maneno ya mazoezi ya viungo,kumbi za mikutano,migahawa na maeneo ya Kisasa ya kuoshea magari.
Kwa upande wake Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya WHI , Sephania Solomon amesema matarajio katika kipindi cha miaka 15 jengo hilo litaingiza zaidi ya sh bilioni15 ambapo Chuo Kikuu itapata asilimia 40 na Taasisi ya Watumishi House itapata asilimia 60.
Amesema WHI imefanya Utafiti kuhusu Mradi huo na inashirikiana na UDSM chini ya mfuko Wa uendeshaji miliki kwa mujibu taratibu.