MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Uchaguzi Mkuu 2025: Majimbo Mapya Nane Yaanzishwa, 12 Yabadilishwa Majina
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Uchaguzi Mkuu 2025: Majimbo Mapya Nane Yaanzishwa, 12 Yabadilishwa Majina
Habari

Uchaguzi Mkuu 2025: Majimbo Mapya Nane Yaanzishwa, 12 Yabadilishwa Majina

Author
By Author
Share
4 Min Read

Na  Mwandishi Wetu,
TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi imeanzisha majimbo mapya nane na kubadilisha majina ya majimbo 12 ya uchaguzi yatakayotumika kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo tarehe 12 Mei, 2025 Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele amesema Tume imefikia uamuzi huo baada ya kupitia maombi kutoka kwenye mikoa mbalimbali nchini.

Amesema uamuzi huo umefanyika kwa kuzingatia masharti ya ibara ya 75(1), (2) na (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 ikisomwa pamoja na kanuni ya 18(7) ya Kanuni za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi za Mwaka 2024.

Ameyataja majimbo hayo kuwa ni Jimbo la Kivule amabalo limegawanywa kutoka Jimbo la Ukonga na Jimbo la Uchaguzi la Chamanzi ambalo limegawanywa kutoka Jimbo la Mbagala yote ya mkoani Dar es Salaam.

“Mkoani Dodoma limeanzishwa jimbo jipya moja, ambapo Jimbo la Uchaguzi la Dodoma Mjini limegawanywa na kuanzishwa jimbo jipya la Uchaguzi la Mtumba na Mkoani Mbeya limeanzishwa jimbo jipya moja, ambapo Jimbo la Uchaguzi la Mbeya Mjini limegawanywa na kuanzishwa Jimbo jipya la Uchaguzi la Uyole,” amesema.

Ameongeza kuwa Mkoani Simiyu limeanzishwa jimbo jipya moja ambapo Jimbo la Uchaguzi la Bariadi limegawanywa na kuanzishwa Jimbo jipya la uchaguzi la Bariadi Mjini.

Jaji Mwambegele amesema Mkoani Geita yameanzishwa majimbo mawili ambapo Jimbo la Uchaguzi la Busanda limegawanywa na kuanzishwa Jimbo jipya la Uchaguzi la Katoro na Jimbo la Uchaguzi la Chato limegawanywa na kuanzishwa Jimbo jipya la Uchaguzi la Chato Kusini.

“Mkoani Shinyanga limeanzishwa jimbo jipya moja, ambapo Jimbo la Uchaguzi la Solwa limegawanywa na kuanzishwa Jimbo jipya la Uchaguzi la Itwangi,” amesema.

Akizungumza kuhusu majimbo kumi na mbili (12) ya uchaguzi yaliyobadilishwa majina, Jaji Mwambegele ameyataja majimbo hayo kuwa ni pamoja na Jimbo la Uchaguzi la Chato ambalo limebadilishwa jina kuwa Jimbo la Uchaguzi la Chato Kaskazini.

“Jimbo la Uchaguzi la Nkenge limebadilishwa jina, sasa litaitwa Jimbo la Uchaguzi la Missenyi, Jimbo la Uchaguzi la Mpanda Vijijini limebadilishwa jina, sasa litaitwa Jimbo la Uchaguzi la Tanganyika na Jimbo la Uchaguzi la Buyungu limebadilishwa jina sasa litaitwa Jimbo la Uchaguzi la Kakonko,” amesema.

Ameongeza kuwa Jimbo la Uchaguzi la Bariadi limebadilishwa jina, sasa litaitwa Jimbo la Uchaguzi la Bariadi Vijijini, Jimbo la Uchaguzi la Manyoni Mashariki limebadilishwa jina na kuwa Jimbo la Uchaguzi la Manyoni na Jimbo la Uchaguzi la Singida Kaskazini limebadilishwa jina na kuwa Jimbo la Uchaguzi la Ilongero.

Majimbo mengine ni Jimbo la Manyoni Magharibi kuwa Jimbo la Itigi, Jimbo la Singida Mashariki kuwa Jimbo la Ikungi Mashariki, Jimbo la Singida Magharibi kuwa Jimbo la Ikungi Magharibi, Jimbo la Tabora Kaskazini kuwa Jimbo la Uyui na Jimbo la Handeni Vijijini kuwa Jimbo la Handeni.

“Kutokana na ongezeko hilo la majimbo nane, kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kutakuwa na majimbo ya uchaguzi 272 yatakayofanya uchaguzi wa wabunge, katika Jamhuri ya Muungano. Kati ya majimbo hayo 222 yapo Tanzania Bara na majimbo 50 yapo Tanzania Zanzibar,” amesema Jaji Mwambegele.

Ameongeza kuwa kutakuwa na kata 3,960 zitakazofanya uchaguzi wa madiwani kwa Tanzania Bara katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

You Might Also Like

Watanzania Washauriwa Kula Senene, Kumbikumbi, Msusa, Ngogwe Kuepuka Udumavu

Majaliwa Ataka Yatolewe Mafunzo Yanayozingatia Soko La Ajira

Watakiwa kuzingatia sheria wanapohudumia walimu

WMA Yajivunia Kuongezeka Kwa Wafanyakzai

Asilimia 22 Ya Vijana Wanakumbwa Magonjwa Yasiyo Ya Kuambukizwa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Serikali Inaboresha Miundombinu Ya Umeme Kibiti Kuondoa Changamoto Za Umeme – Kapinga
Next Article Wanafunzi Msingi Wajitosa Kujifunza Kichina
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

SUA Yawafikia Wafugaji Wa Ng’ombe Wa Maziwa Kwa Tiba Mbadala Ya Homa Ya Kiwele
Habari May 12, 2025
Wanafunzi Msingi Wajitosa Kujifunza Kichina
Habari May 12, 2025
Serikali Inaboresha Miundombinu Ya Umeme Kibiti Kuondoa Changamoto Za Umeme – Kapinga
Habari May 12, 2025
Waziri Mkuu Kumwakilisha Dkt Samia Ivory Coast
Habari May 12, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?