MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TSB, Wizara ya kilimo yaweka mpango wa vituo vya usindikaji mkonge
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TSB, Wizara ya kilimo yaweka mpango wa vituo vya usindikaji mkonge
Habari

TSB, Wizara ya kilimo yaweka mpango wa vituo vya usindikaji mkonge

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: MPANGO wa kuweka vituo vya usindikaji wa zao la mkonge umewekwa  kwa lengo la kumsaidia mkulima mdogi ili aweze kusindika na kupata nyuzi Singapore ambazo zitakubalika katika soko la ndani na nje ya nchi.
Mpango ambao umewekwa na Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo.
Mkuu sehemu ya Maendeleo ya mkonge kutoka TSB,Simon Kibasa, amesema hayo katika maonesho ya wakulima, Wafugaji na Wavuvi yanayofanyika  Kitaifa viwanja vya nane nane Nzuguni jijini Dodoma.
Kibasa amesema Bodi imekuwa ikiwaunganisha wakulima na masoko na kwamba  sehemu ya  masoko hayo ni  kuwaunganisha  wakulima hao ili wapate soko la bei nzuri.
Ameongeza kuwa nchini Tanzania wakulima wamegawanyika katika makundi matatu wadogo, wakubwa na wakati  huku akisema  wakulima wakubwa hawana changamoto kama ilivyo kwa wakulima hao wadogo.
“Na wakulima wadogo nao wamegawanyika katika sehemu mbili wanaolima kwenye mashamba yao binafisi na wanao fanyabiashara  lakini wapo ambao wanalima  kilimo cha mkataba kinachoendeshwa katika mashamba matano nchini yakiwamo Ngombezi na magoma,” amesema.
Amefafanua kuwa katika mashamba hayo yana mikataba kati ya mkulima mdogo na Bodi ambapo inamkodisha mkulima huyo na kazi yake ni kulima na kutunza mkong na kwamba kuna mkataba kati ya vyama vya ushirika vilivyopo katika mashamba hayo na usindikaji.
“Wote hawa wanasimamiwa na Bodi kwa kushirikiana na ofisi ya Msajili wa vyama vya ushirika Mkoa wa Tanga katika maeneo hayo TSB imekuwa ikiwasimamia wakulima kuhakikisha wanapata bei nzuri kupitia wanunuzi mbalimbali.
Kibasa ameongeza kuwa lengo la kuhamasisha kilimo hicho ni zao ambalo lina soko kubwa na ni zao ambalo linastamili magonjwa, ukame na ni la uhakika kumpatia mkulima kipato.
Bodi hiyo ni Taasisi ya serikali ambayo ipo chini wizara ya kilimo ni msimamizi na mhamasishaji maendeleo ya mkonge nchini.

You Might Also Like

Programu Ya Samia Extended Scholarship Yazinduliwa

RAAWU yapokea migogoro 16, yaishughulikia

UDSM  Kujenga Jengo La Kisasa La Bil 8.3

Trump Amteua Mtendaji Mkuu White House, Safari Ya Kuunda Timu Yake

Majaliwa Asisitiza Matumizi ya Mifumo ya Kieletroniki Katika Makusanyo

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Mikoa mitatu kuanzishwa vituo vya gesi asilia
Next Article Marekebisho ya sheria huangalia mazingira ya sasa na yajayo – Tume
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Waziri Mkuu Majaliwa Akabidhi Tuzo kwa BoT Geita
Habari September 22, 2025
BoT Yarahisisha Uuzaji wa Dhahabu kwa Wachimbaji, Yatoa Punguzo La Mrabaha
Habari September 22, 2025
Waziri Mkuu Apongeza Huduma Kidijitali za NSSF, Maonesho Ya Madini Geita
Habari September 22, 2025
Mkuu Wa Mkoa Shinyanga Asifu Kazi Ya Bodi Bima Ya Amana
Habari September 22, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?