MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TPHPA Yapata Tuzo ya WCO kwa Ulinzi wa Afya na Usalama wa Taifa
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TPHPA Yapata Tuzo ya WCO kwa Ulinzi wa Afya na Usalama wa Taifa
Habari

TPHPA Yapata Tuzo ya WCO kwa Ulinzi wa Afya na Usalama wa Taifa

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read

Na Lucy Ngowi

DAR ES SALAAM: MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), Profesa Joseph Ndunguru, amesema mamlaka hiyo inaendelea kuchangia ukusanyaji wa mapato ya Serikali na kulinda nchi dhidi ya uingizaji wa bidhaa zisizokidhi viwango, hususan mazao na viuatilifu hatarishi.

Habari Picha 10954

Amesema TPHPA imekuwa mstari wa mbele kuwezesha ufunguaji wa masoko ya mazao yanayosafirishwa nje ya nchi, sambamba na kuhakikisha mazao yanayoingia au kupita nchini hayana visumbufu kama magonjwa na wadudu waharibifu wa mazao.

Profesa Ndunguru amepongeza ushirikiano uliopo kati ya TPHPA, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na taasisi nyingine za udhibiti, hasa katika ofisi za mipakani, nchi kavu, bandari na viwanja vya ndege ambako TPHPA ina ofisi 44.

Amesema ushirikiano huo umeimarisha utekelezaji wa majukumu ya mamlaka na kuchangia kukuza uchumi wa Taifa kupitia biashara halali na salama.

Ameeleza hayo muda mfupi baada ya TPHPA kutunukiwa cheti cha kutambua mchango wake na Shirika la Forodha Duniani (WCO) katika hafla iliyoandaliwa na TRA na kufanyika katika Kumbi za Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

Taarifa ya mamlaka hiyo imeeleza kuwa tuzo hiyo imetolewa kutokana na mchango wa TPHPA katika kulinda afya ya binadamu, mimea na mazingira dhidi ya athari za matumizi yasiyo salama ya viuatilifu, pamoja na usimamizi madhubuti wa uingizaji na usambazaji wake nchini.

TPHPA imetoa shukrani kwa WCO, TRA na wadau wote, ikiahidi kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi na ufanisi kwa maslahi ya Taifa.

Habari Picha 10955
Habari Picha 10953

You Might Also Like

BoT Yawaalika Wachimbaji Kuwekeza Serikalini, Yatoa Elimu ya Fedha

Mchumi Ajitosa Kuwania Ubunge Manyoni

Waziri Mkuu Mstaafu Pinda Atoa Neno Kwa Vijana, Maadhimisho Miaka 30 VETA

BRELA Yazindua Baraza La Wafanyakazi

Watumishi REA Watakiwa Kufanya Kazi Kuendana Na Kasi Ya Serikali

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Dira za Maji Kumaliza Kero ya Ankara
Next Article Dkt. Majule Ahoji Hatua za Kulinda Wananchi Dhidi ya Mikopo Hatari
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mbunge Asisitiza Sheria za Majiko Safi Ili Kulinda Mazingira
Habari February 3, 2026
Mwalunenge: Bila Rasilimali Watu Na Mtaji, Mipango Ya Kilimo Haitafanikiwa
Habari February 3, 2026
Gulamali Ahoji Bungeni Changamoto ya Mawasiliano Ilongelo
Makala February 3, 2026
Serikali Yaendelea Kuimarisha Uhuru wa Mahakama – Nchimbi
Habari February 2, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?