MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Tido Mhando: Marufuku Kuwasilisha Vyeti, Nyaraka Za Kughushi Maombi ya Ithibati, Press Card
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Tido Mhando: Marufuku Kuwasilisha Vyeti, Nyaraka Za Kughushi Maombi ya Ithibati, Press Card
Habari

Tido Mhando: Marufuku Kuwasilisha Vyeti, Nyaraka Za Kughushi Maombi ya Ithibati, Press Card

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: MWENYEKITI wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Tido Mhando amesema Waandishi wa habari watakaobainika wamewasilisha vyeti au nyaraka za kughushi katika ujazaji wa vitambulisho kwa njia ya mtandao, watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Hatua hizo zitajumuisha kufutiwa mara moja usajili wao, ikiwa ni pamoja na kufikishwa katika vyombo vya sheria kwa ajili ya kuchukuliwa hatua stahiki,
Pia kupigwa marufuku kujihusisha na shughuli za uandishi wa habari  au majukwaa mengine ya kitaaluma.
Mhando amesema hayo leo Mei 19, 2025 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu uzinduzi rasmi wa maombi ya Ithibati na vitambulisho vya wana habari vijulikanavyo kama Press Card.
Amesema, “Bodi imekaa vizuri hatutapenda tuchezewe katika hilo. Mtu akisema anafanya najaribio, akaingia katika hali ambayo inamhuzunisha asituhukumu. Sisi tutafuata vigezo vinavyoeleweka,”.
Ameonya tabia ya vyuo vinavyojiandaa kutoa au tayari vimetoa vyeti vya kughushi visijaribu kufanya hivyo kwa kuwa lengo la JAB ni kuipa heshima fani ya habari.
“Wakati umefika wa kuheshimisha tasnia yet. Tunataka watu watuheshimu kama tasnia nyingine zinavyoheshimika.
“Kumekuwa na taarifa zinazodokeza kuwepo kwa baadhi ya watu wanaojaribu kuwasilisha vyeti vya kughushi au nyaraka zisizo halali kwa lengo la kujipatia usajili na vitambulisho kinyume na taratibu.
“Tunapenda kusisitiza kuwa jambo hilo si tu linakiuka maadili ya taaluma ya habari, bali pia ni makosa ya jinai yanayoadhibiwa kwa mujibu wa sheria za nchi,” amesema.
 Mfumo wa TAI HABARI umeanzishwa kwa nia njema ya kuimarisha taaluma ya uandishi wa habari kwa misingi ya uwajibikaji, weledi na heshima.
Amesema lengo likiwa ni kuhakikisha kila mwandishi aliyesajiliwa ni mtu mwenye sifa stahiki, mafunzo sahihi, na anayezingatia maadili ya kazi hiyo muhimu kwa jamii.
“Kwa mantiki hiyo, nyaraka zote zinazowasilishwa zitahakikiwa kwa kina kwa kushirikiana na taasisi husika na hivyo basi, udanganyifu wowote utabainika.
“Tunatoa wito kwa waandishi wa habari wote kuwa waaminifu na waadilifu katika hatua zote za kujisajili kwa kutambua kuwa taaluma ya habari ni mhimili muhimu katika jamii yoyote, na uhai wake unategemea maadili ya wale wanaoitekeleza.
“Tujiepushe na tamaa au njia za mkato ambazo zinaweza kuharibu sifa binafsi na kuchafua taswira ya tasnia nzima ya habari,” amesema.

You Might Also Like

TIB Yaanda Mkakati Kabambe Wanawake Kuchangamkia Fursa

Kabonaki: Jiungeni Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Hiari

TPHPA ina mchango mkubwa utoshelevu wa chakula – Profesa Ndunguru

Dendego Achangisha Bilioni 1.7, Ujenzi Ofisi Ya CCM

Tanzania kujiimarisha zaidi kidiplomasia – Majaliwa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Shen Zhiying: Mkongwe Aliyeanzisha Kozi Ya Kiswahili Nchini China
Next Article Watanzania Watakiwa Kufanya Kazi Kwa Bidii
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

JAB Yaanza Rasmi Kutoa Vitambulisho Kwa Waandishi Wa Habari
Habari May 19, 2025
Hivi Ndivyo Vipaumbele Vya Maliasili
Habari May 19, 2025
Watanzania Watakiwa Kufanya Kazi Kwa Bidii
Habari May 19, 2025
Shen Zhiying: Mkongwe Aliyeanzisha Kozi Ya Kiswahili Nchini China
Makala May 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?