Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM: TAASISIi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, imetoa mafunzo mbalimbali kwa Chama cha Waendesha Bajaji na Bodaboda katika Manispaa hiyo.
Mafunzo hayo yameongozwa na Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Ubungo, Devotha Mihayo katika ukumbi wa Stazia mapema Leo Februari 26, 2025.

Akizungumza katika jukwaa hilo la Maofisa Usafirishaji wa Kata ya Msigani.Mihayo amesisitiza juu ya umuhimu wa kufanya shughuli kwa kufuata kanuni na taratibu za serikali, kujiepusha na vitendo vya Rushwa, kujali Afya zao pamoja na kuchangia mapato ya Halmashauri
“Maafisa usafirishaji mnalo jukumu la kujiunga vikundi ili serikali iweze kuwawezeshe kwenye shughuli zenu huku mkihakikisha mnajali na fya zenu kwa kuwa na bima za Afya,” amesema.

Awali Meneja wa chanzo cha maegesho Manispaa ya Ubungo, Pascal Peter amewataka maofisa usafirishaji hao kuhakikisha wanalipia ada zao za maegesho ili kuwa na sifa zote za kupata fursa mbalimbali ikiwemo fursa kubwa ya mikopo.
Vigezo vya kikundi kupata usajili wa maegesho ya kikundi ni pamoja na kuwa na TIN namba ya kikundi, katiba ya kikundi, barua ya kuomba usajili, kikundi kuwa na uongozi pamoja na sare.
Ada ya Kila mwanachama katika kikundi ni Sh. 30,000 kwa mwaka
Naye Ofisa maendeleo kata ya Msigani, Belia Benjamin ameeleza namna ya kupata mikopo ya asilimia 10 isiyo na riba ni kujiunga katika vikundi vya watu watano mpaka 30, kuwa na katiba, vitambulisho vya NIDA pamoja na usajili wa vikundi.
Mkutano huo umehudhuriwa na Mtendaji Kata ya Msigani, Ofisa Maendeleo ya Jamii Msigani, Maofisa Biashara, Viongozi wa Chama cha Bajaji na bodaboda pamoja na wanachama wao.