Na Mwandishi Wetu
MASWA MAGHARIBI: MGOMBEA ubunge wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), John Shibuda, amewataka WanaMaswa kujitokeza bila woga kukata rufaa ya maisha yao Oktoba 29 mwaka huu.
Akimkaribisha jimboni humo mgombea urais wa CHAUMMA, Salum Mwalim, Shibuda amewataka wananchi waamke na kuuondoa umaskini uliotengenezwa na chama tawala tangu uhuru.
“Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alisema hatuwezi kutatua matatizo yetu kwa kujidanganya kuwa hayapo. Nichagueni nikayasemee matatizo ya kijamii na kiuchumi yanayoikwaza jamii na uchumi, maana dawa ya jino bovu ni kung’oa,” amesema.



