MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Serikali Yazindua Mafunzo Ya Mtandao Ya Afya Moja
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Serikali Yazindua Mafunzo Ya Mtandao Ya Afya Moja
Habari

Serikali Yazindua Mafunzo Ya Mtandao Ya Afya Moja

Author
By Author
Share
4 Min Read

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imeanzisha mafunzo kwa njia ya mtandao ya Afya moja (ECHO) ili kuwajengea uwezo watoa huduma wa kada za afya ya binadamu, wanyama na mazingira kwa ngazi zote.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Dkt Jim Yonazi wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo katika Kituo cha kurushia Mafunzo kwa njia ya mtandao (ECHO HUB) kilichopo katika jengo la Idara ya Utafiti na Mafunzo Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

Amesema Serikali inaendelea kukabiliana na majanga na dharura zenye athari kwa afya ya binadamu, wanyama na mazingira hivyo imeona umuhimu wa kuwezesha wataalamu wake kuelewa kwa kina dhana ya Afya Moja.

“Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Wizara za Kisekta na mradi wa USAID Usalama wa Afya Duniani unaotekelezwa na Shirika la CIHEB Tanzania, imeanzisha mafunzo ya mtandao ya Afya moja (ECHO) ili kujenga uwezo kwa watoa huduma wa kada za afya ya binadamu, wanyama na mazingira kwa ngazi zote,”amesema Dkt. Yonazi.

Ameongeza kuwa; “Naomba niwahamasishe viongozi na watumishi kutoka sekta mbalimbali kushiriki katika vipindi hivi. Wataalamu wabobezi watawasilisha mada mbalimbali zitakazojenga uwezo wetu katika kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na magonjwa ya mlipuko kwa binadamu na wanyama, visumbufu vya mazao, usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa, usalama wa chakula.

 

Awali akieleza lengo la uzinduzi wa mafunzo hayo Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Brigedia Generali Hosea Ndagala amesema,Mafunzo haya yanalenga katika kuongeza ufanisi kwa wataalam katika kushughulikia magonjwa ya kizoonotiki, usugu wa vimelea dhidi ya dawa (AMR), hatari za kibailojia, usalama wa chakula na magonjwa yasiyoambukizwa ambayo ni maeneo muhimu yenye changamoto na yanapewa kipaumbele katika Sekta ya Afya nchini Tanzania.

Amefafanua kuwa, Mafunzo haya yatawahusu wataalamu wa Sekta ya Afya moja, Afya, mazingira, mifuko na uvuvi.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Afya na Lishe Ofisi ya Rais-TAMISEMI Suzanne Nchalla amesema mpango huo utasaidia watoa huduma ngazi ya msingi kupata uelewa wa Dhana ya Afya Moja na wakati wa utoaji huduma.

Amesema OR- TAMISEMI itashirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu katika kuhakikisha watumishi wa afya ya msingi wanashiriki kikamilifu katika mafunzo hayo.

“Tutawasimamia na kuwakumbusha viongozi wa Halmashauri kuhakikisha wanashiriki vipindi vilivyopangwa ili kupata matokeo chanya na kutimiza azma la mpango huu,”amesema .Suzanne.

Naye Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Serikali Dkt.Otilia Gowelle amesema Wizara ya Afya inatambua umuhimu wa mashirikiano ya wadau na sekta mbalimbali katika kujiandaa pamoja na kukabiliana na matishio ya mara kwa mara ya magonjwa ya mlipuko pamoja na matukio yenye athari kwa afya ya binadamu.

“Kwa kuzingatia umuhimu wa mafunzo haya, Wizara imekwisha fanya uhamasishaji na itaendelea kuhakikisha wataalam wengi zaidi wanashiriki mafunzo haya wakiwemo wauguzi, madaktari, wafamasia, maofisa afya, wataalam wa maabara na wengineo waliopo katika vituo vya kutolea huduma na maeneo mengine mahsusi” amesisitiza Dkt. Gowelle.

Ameongezea kuwa Wizara ya Afya imekuwa mshiriki na mnufaika mkuu wa ushirikiano uliopo kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano kila inapohitajika.

You Might Also Like

Serikali yatambua deni la Kiwira Coal Mine Bill.1.52

NIT Yasema Ina Uwezo Wa Kufundisha Kozi Ya Urubani

Ulega: Miaka 50 ya ILRI imeinufaisha Tanzania 

Dkt. Biteko ashiriki kilele cha miaka 60 JWTZ

Kafulila: Deni La Taifa Ni Himilivu

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Watu Zaidi Ya 3500 Wapatiwa Huduma Ya Kisheria Wizara Ya Katiba Na Sheria
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Watu Zaidi Ya 3500 Wapatiwa Huduma Ya Kisheria Wizara Ya Katiba Na Sheria
Habari July 16, 2025
Ubunifu Na Kufanya Tafiti Kwawezesha UDOM Kupokea Tuzo
Habari July 16, 2025
Utafiti Wa Nguvu Kazi, Mapato Ya Kaya Kutoa Taswira Mpya Ya Maendeleo
Habari July 15, 2025
Majaliwa Aituza UDSM kwa Kuongoza Eneo La Elimu, Utafiti, Ubunifu Sabasaba 2025
Habari July 14, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?