Na Lucy Lyatuu
KATIKA kuchochea uwekezaji unaoleta tija zaidi na kutoa fursa kwa vijana serikali ina mpango wa kuanzisha kituo maalum cha kuhudumia na kuwezesha wawekezaji vijana.
Aidha itaanzisha program maalum ya kuwezesha wawekezaji vijana kubuni na kuanzisha uwekezaji wa viwanda nchini kote.
Waziri kutoka Ofisi Ya Rais, Mipango Na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema hay oleo Dar es Salaam wakati akieleza vipaumbele na fursa kwa vijana katika miaka mitano ijayo na kuongeza kuwa programhiyo itazinduliwa kabla ya mwisho wa mwaka.
Amesema katika kuwezesha mipango hiyo kwa kuanzia watatenga maeneo ambayo vijana waliomaliza vyuo vikuu na vyuo vyuo vya ufundi kupewa ili kuweza kuwekeza kwenye viwanda.
Profesa Kitila amesema program hiyo itahusisha mafunzo, uwezeshaji wa kupewa ardhi, kuunganishwa na wauzaji wa mitambo na malighafi na pia kuunganisha na benki ambazo zina ushirikiano na TISEZA.
“Tutatenga maeneo yafuatayo maalum kwa uwekezaji utakaofanywa na vijana,” amesema na kuyataja maeneo hayo na ardhi itakayotumika kuwa ni pamoja na Dodoma eneo la Nala lenye ekari 100.
Ameyataja maeneo mengine kuwa ni Pwani eneo la Kwala ekari 20, Mara (Bunda) ekari 100, Ruvuma (Songea) ekari 100 na Bagamoyo ekari 20 .
Mbali na kuanzisha program hiyo, Profesa Kitila amesema serikali ina mpango wa kusogeza huduma za Mamlaka ya uwekezaji na maeneo maalum ya kiuchumi kufikia kila mkoa ifikapo mwaka 2028.
Amesema kila mkoa utakuwa na kituo maalum cha kutangaza na kuwezesha wawekezaji Pamoja na agizo la Rais Dkr Samia Suluhu Hassan la kusogeza huduma kwa wananchi wote.
“Tutashirikiana na TAMISEMI kuratibu na kuwezesha huduma hizi kuwafikia wote nchini,” amesema Profesa Kitila an kuongeza pia kwa kushirikiana na sekta binafsi kujenga miundombinu ya uwekezaji wa viwanda nchi nzima.
Amesema kwenye eneo hilo TISEZA ataingia ubi ana wenye mitaji ili kujenga majengo ya viwanda ambayo yatakodishwa kwa gharama nafuu kwa mtanzania yoyote anayetaka kuwekeza kwenye viwanda.
Amesema mpango utapunguza gharama za watanzania kuwekeza na kunufaika na mageuzi ya kiuchumi yanayotokea nchini kote, hatua hiyo itaongeza fursa za kiuchumi na kukuza kipato cha mtanzania mmojammoja.
Profesa Kitila amesema pia serikali itabuni na kuanzisha vituo vipyavya kiuwekezaji mara kwa mara ili kuongeza uimara wa uwekezaji nchinina mvuto wa Tanzania kwa wote wenye mitaji huko duniani.
“ Katika kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini, serikali inakamilisha maadalizi ya mkakati mpya wa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini utakaozinduliwa kabla ya kuanza utekelezaji wa dira 2050 Julai mosi 2026.
Amesema ni matarajio ya serikali ifikapo mwaka 2030 hatua kubwa zitakuwa zimepigwa na mfanikio makubwa kupatikana ikiwemo kuongezeka miradi ya uwekezaji, fursa za ajira kupanuka na mitaji ya uwekezaji kukua.
Amesema matarajio ni kuzalisha ajira milioni nane na kuvutia mtaji wenye jumla yad ola za Kimarekani angalau bilioni 50 ifikapo 2030.

