Na Danson Kaijage
DODOMA: RAIS Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Mkutano Mkuu wa 39 wa mwaka wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania ( ALAT), utakaofanyika Aprili 17 hadi 21., mwaka huu 2025 jijini Mwanza.
Katibu Mkuu wa ALAT Taifa,
Mohammed Maje amesema hayo wakati wa kikao kazi kilichohusisha makatibu wa mikoa wote ambapo lengo likiwa ni kuweka mikakati kufanikisha mkutano huo.

Amesema ili kufanikisha mkutano huo, mshikamano ndani ya Jumuiya hiyo ni muhimu kwa kuwa hakuna taasisi ambayo inaweza kuendelea bila kuwa na umoja.
Amesema pamoja na kuweka mikakati ya kufanikisha mkutano huo, pia kikao kilichofanyika kililenga kuimarisha mahusiano ya kiutendaji na matawi yake ya mikoa, wilaya pamoja na Kata.