Na Mwandishi Wetu Kasulu
KIGOMA: MAELEKEZO ya Rais Samia Suluhu Hassan yanayotaka utumikaji wa 4R katika shughuli zote za kitaifa zinazoakisi maridhiano, mabadiliko, ustahimilivu na kujenga upya yamewezesha kufanikiwa kwa uandikishwaji katika Daftrari laMpiga Kura Kasulu.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Kigoma Dkt, Semistatus Mashimba amesema hayo alipozungumza na Waandishi wa Habari.

Amesema kupitia misingi hiyo katika mchakato huo mzima wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na uandikishaji katika wilaya hiyo wameshirikiana na viongozi wote wa chama na serikali,vyama vyote vya siasa, makundi ya wazee maarufu, vijana na vikundi vya sanaa ili kuhakikisha unafanikiwa.
Ametaja jambo lingine ni kuzingatia miongozo waliyopewa na viongozi mbalimbali kuanzia ngazi ya mkoa,wilaya pamoja na halmashauri,

Vilevile miongozo na kanuni iliyoratibiwa vizuri na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI
iliyosaidua vifaa na fedha kufika kwa wakati hali iliyosababisha mchakato kutokuwa na dosari.
Pia amevishukuru Vyombo vya Habari wilayani hapo
kwa hamasa kubwa waliyoitoa iliyochangia wananchi kwenda kujiandiskisha,