Na Mwandishi Wetu
SONGWE: WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete yupo mkoani Songwe kwa ajili ya kukagua miradi ya maendeleo ya Sekta ya Elimu, Afya na Miundombinu kwa ajili ya ustawi wa maendeleo ya wananchi.
Ridhiwani katika ziara yake hiyo ataweka mawe ya msingi katika miradi hiyo inayokadiriwa thamani ya zaidi ya Sh. Bilioni 700 katika Halmashauri zote za mkoa huo.
Vile vile Waziri Ridhiwani atakagua Maendeleo ya Kituo cha Vijana cha Sasanda wilayani Songwe ya mradi wa Shamba la vijana lililopo kituo hicho.
Katika ziara hiyo, Ridhiwani ameambatana na watendaji mbalimbali ambao wako tayari kwa kazi iliyowapeleka.
Baada ya kuwasili mkoani hapo, Ridhiwani alipokelewa na Mkuu wa Mkoa huo, Daniel Chongolo na kumjulisha hali ya maendeleo ya Mkoa huo na maandalizi ambayo yameshafikiwa kwa ajili ya ziara hiyo.