Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila wiki ijayo siku ya Jumanne, ataandamana na wasaidizi wake, kwenda kuzungumza na Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa kwa ajili ya kujadili namna ya kuwepo Safari za treni ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam.
Chalamila amesema hayo leo alipozungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na mafanikio yaliyopatikana wakati wa mkutano wa nishati.
Amesena, ” Na kwa matinki hiyo Jumanne ya wiki ijayo, tutakaa kikao cha pamoja na Mtendaji Mkuu wa TRC Masanja Kadogosa, pamoja na wakurugenzi wetu, Ma Das na wakuu wa wilaya ili kujadiliana.
” Tutajadiliana Namna ya kujenga reli ya kawaida inayobeba abiria,” amesema.
Amesema hiyo itasaidia kuendelea kupunguza msongamano .