Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema Dar es Salaam ina uhitaji wa kuwa na reli za ndani ya mji ili kusafirisha wakazi wake ili kupunguza msongamano.
Chalamila ameeleza hayo wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kipande cha saba na nane Uvinza Malagarasi hadi Msongati nchini Burundi.
Amesema, ” Barabara za mwendo kasi hazitatosha, tufikirie namna ya kuingia kwenye ubia tuwe na reli zitakazochukua watu hapa mjini,”.
Amesema ubia huo utashirikisha halmashauri za Dar es Salaam na wadau wa sekta binafsi.
Akizungumzia mradi huo amesema wananchi wa Dar es Salaam, wanafarijika na mradi huo.
Pia kufika reli hiyo ya Kisasa nchini Burundi itapunguza msongamano wa mizigo mkoani Dar es Salaam.
” Uwepo wa reli hii utasaidia wananchi wa Burundi kutofika Dar es Salaam ili kuchukua mizigo yao badala yake wataichukulia Kigoma,” amesema.