MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: PURA, M&P zajadili mradi wa uchorongaji visima vya gesi Mnazi Bay
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Uncategorized > PURA, M&P zajadili mradi wa uchorongaji visima vya gesi Mnazi Bay
Uncategorized

PURA, M&P zajadili mradi wa uchorongaji visima vya gesi Mnazi Bay

Penina Malundo
By Penina Malundo
Share
2 Min Read

Na Mwandishi wetu

Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imefanya mazungumzo na mwendeshaji wa Kitalu cha Mnazi Bay (Kampuni ya Maurel et Prom Exploration Production Tanzania Ltd) kujadili mradi wa uchorongaji wa visima vitatu vya gesi asilia unaotarajiwa kutekelezwa mwanzoni mwa mwaka 2025.

Mazungumzo hayo yamefanyika leo, Septemba 30, 2024 katika Ofisi za PURA Dar es Salaam chini ya uenyekiti wa PURA.

Miongoni mwa wajumbe walioshiriki kikao hicho ni pamoja na Bw. Simon Nkenyeli ambaye ni Meneja wa Utafutaji na Uzalishaji wa Mafuta na Gesi Asilia kutoka PURA na Meneja Mkuu wa M&P Bw. Sylvain Pichelin.

Katika kikao hicho, M&P ilitoa ufafanuzi wa bajeti ya mradi, hatua muhimu kabla ya PURA kutoa idhini ya matumizi ya fedha kwa ajili ya mradi huo. Mradi unatarajiwa kugharimu Dola za Marekani Milioni 80.2

Kati ya visima vitakavyochimbwa, visima viwili (MB5 na MS2) vitakuwa visima vya uzalishaji (_infill_) wakati kisima kimoja (Kasa) kitakuwa kisima cha utafutaji.

Kuelekea utekelezaji wa mradi, tathmini ya athari kwa mazingira imekamilika na zoezi la fidia kwa wananchi watakaopisha mradi linatarajiwa kuanza mapema mara baada ya uhakiki kukamilika.

PURA na M&P zilijadilia pia ushiriki wa watanzania na watoa huduma wa kitanzania katika zabuni zinazotokana na mradi huo.

Katika eneo hili, PURA iliitaka M&P kuhakikisha inazingatia matakwa ya Sheria kuhusu ushiriki wa watanzania. Aidha, PURA ilieleza kuwa inafuatilia kwa karibu kila hatua ya utekelezaji wa mradi huo kuhakikisha watanzania na watoa huduma wa kitanzania wanashiriki kikamilifu.

Kitalu cha Mnazi Bay kina visima vitano vinavyozalisha gesi asilia kwa wastani wa futi za ujazo milioni 74.24 kwa siku (kwa mwezi Septemba)

Wabia katika Kitalu hicho kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara ni M&P (ambaye ni mwendeshaji) mwenye ushiriki wa asilimia 60 katika shughuli za uzalishaji na TPDC mwenye asilimia 40.

Uchorongaji wa visima vitatu vipya utawezesha kuimarisha uzalishaji (maintenance of production plateau) na kuwezesha upatikanaji wa taarifa za kijiolojia kuhusu mashapo yaliyo katika Kitalu hicho.

You Might Also Like

Hakuna Vituo Bandia vya Kuandikisha Wapigakura:Mchengerwa

Wananchi Wachagua Viongozi Serikali Za Mitaa

Mbunge Wa Kibamba Mtemvu. Ajitokeza Kujiandikisha, Kuboresha Taarifa Zake

Kapinga : Bei ya umeme Tanzania ni nafuu kuliko nchi nyingine Afrika Mashariki

Waziri Pinda ashiriki mazishi ya Jaji Kipenka

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Profesa Mutembei apongeza serikali kuruhusu mchepuo lugha ya kichina
Next Article
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?