Na Lucy Ngowi
DODOMA:WANACHAMA wa Mfuko wa Pensheni wa Wastaafu (PSSSF), wamerahisishiwa kupata huduma kwa kuwa sasa mfuko huo upo kidijitali.
Ofisa Matekelezo Mwandamizi wa mfuko huo, Innocent Sizulwa amesema hayo katika maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi yanayoendelea jijini Dodoma.
Amesema mfumo huo wa kidijitali sasa utawawezesha wanachama wake kupata huduma mbalimbali za mfuko bila kufika ofisini.
Sizulwa amesema mfumo huo utawasaidia kupata taarifa kwenye simu zao za mkononi kwa.maana ya simu janja .
“Kupitia mfumo huo na kwa kutumia simu janja ,mteja atapata huduma zote ikiwemo taarifa za michango yake ,kusajili mafao,kuongezea taarifa mbalimbali za kiuanachama kama idadi ya watoto na wategemezi katika mfuko,” amesema.
Amesema ili kujiunga katika mtandao huo,mwanachama anapaswa kuwa na namba ya simu,sahihi na namba ya utambulisbo wa Taifa.
“Mfumo huu sasa humwezesha mteja kufanya shughuli za PSSSF akiwa nyumbani.
Kwa upandewake Ofisa Mawasiliano, Rehema Mkamba amesema PSSSF imewekeza kwa wadau bidhaa za ngozi kwenye kiwanda cha Kilimanjaro ambacho hutengeneza viatu, mikanda, mikoba na kuuza kwa wateja wao..
Vile vile ameaema mfuko umewekeza kwenye ranchi za kisasa ya Nguru ya Mvomero