ADDIS ABABA, ETHIOPIA: MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), Profesa Joseph Ndunguru, ameongoza kikao cha 70 cha Baraza la Mawaziri wa Shirika la Kudhibiti Nzige wa Jangwani Ukanda wa Afrika Mashariki (DLCO–EA), kinachofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Profesa Ndunguru amemwakilisha Waziri wa Kilimo wa Tanzania, Hussein Bashe, na ndiye Mwenyekiti wa kikao hicho.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu (TOSCI), Nyasebwa Chimagu, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya shirikisho hilo, naye ameshiriki kikao hicho pamoja na wajumbe wengine kutoka nchi wanachama wa DLCO–EA.
