MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Mtanda Akagua Maendeleo Ya Mradi YA Hoteli Ya Nyota Tano Ya NSSF
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Mtanda Akagua Maendeleo Ya Mradi YA Hoteli Ya Nyota Tano Ya NSSF
Habari

Mtanda Akagua Maendeleo Ya Mradi YA Hoteli Ya Nyota Tano Ya NSSF

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Mwandishi Wetu
MWANZA:  MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, amekagua maendeleo ya ujenzi wa Hoteli ya Nyota Tano ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), inayojengwa katika eneo la Capripoint jijini Mwanza.
Hoteli hiyo itaendeshwa na Kampuni ya Kimataifa ya Radisson.
Katika ziara hiyo, Mtanda amesema ameangalia chumba cha mfano kilichojengwa na kampuni ya Radisson ambacho kitakuwa mfano wa vyumba vingine vyote 183 vinavyoendelea kujengwa kwa ubora wa hali ya juu.
“Nimefarijika kuona maendeleo ya ujenzi yakiendelea kwa ubora wa hali ya juu.
“Leo nimeona chumba cha mfano kati ya vyumba 183 vinavyotarajiwa kukamilika, vyote vikiwa na muonekano mmoja ambao unaangalia Ziwa Victoria.
“Kukamilika kwa hoteli hii kutaliwezesha jiji letu kuwa na miundombinu ya kisasa ya kupokea wageni wa kitaifa na kimataifa,” amesema.
Ameipongeza NSSF kwa uwekezaji wa mradi huo na kwamba ameona viwango vya mwendeshaji wa hoteli hiyo kuwa vinavutia ikiwemo chumba hicho cha mfano.
Mtanda ameishukuru Serikali kwa kuruhusu mradi huo kuendelea.
“Kwa hiyo nawapongezeni sana NSSF kwa uwekezaji huu mkubwa ambao ukikamilika utakuwa na tija kubwa kwa uchumi wa Kanda ya Ziwa, kuimarisha sekta ya utalii na kufungua fursa mpya za ajira kwa wananchi,” amesema.
Amesema kupitia mradi huo na mingine ya kimkakati kama vile uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwanza, meli ya Mv. Mwanza na reli ya SGR, jiji hilo litafikika kwa urahisi na kuwa kivutio kikuu cha uwekezaji na utalii kwa upande wa Kanda ya Ziwa.
Amesema kwa sasa Mkoa wa Mwanza unachangia asilimia 7.2 katika pato la Taifa, lakini kutokana na miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa ukiwemo wa hoteli hiyo, mchango huo unaweza kufikia asilimia 10.
Akielezea umuhimu wa uwekezaji huo, Mtanda amesema uwepo wa hoteli ya kiwango cha kimataifa ni hitaji la msingi kwa miji inayokua haraka kama Mwanza, utakapokamilika utachochea fursa za kiuchumi na kukuza utalii.
Naye Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Miradi wa NSSF,  Gabriel Silayo, amesema mradi huo umefanyiwa utafiti wa kina na utaleta faida kwa Mfuko na Taifa kwa ujumla.
“Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa, nikuhakikishie kuwa tumefanya utafiti na tumeona kuwa mradi huu utalipa. Kama ulivyojionea tumempata wendeshaji wa kimataifa Radisson ambaye ana hoteli zaidi ya 12,000 duniani kote, zikiwemo zaidi ya 98 barani Afrika”, amesema.
Kwa upande wake, Meneja wa Mradi huo kutoka Afrika Kusini, Gehan Nel amesema atahakikisha anasimamia mradi vizuri ili kukidhi ubora wa hoteli zingine za Radisson  duniani na amepongeza serikali ya Tanzani kwa kuruhusu wawekezaji kuja kuwekeza nchini.
Amesema kwa kushirikiana na NSSF atasimamia mradi huo ili ukamilike kwa haraka kwani hoteli hiyo imejengwa katika mandhari ya kuvutia kando ya Ziwa Victoria na itachochea wageni wengi kufika nchini.
Uwekezaji huu ni moja kati ya majukumu ya Mfuko wa NSSF kuwekeza sehemu mbalimbali ili kuhakikisha inalinda thamani ya michango ya wanachama.

You Might Also Like

Ajali ya treni Kigoma , abiria 70 wajeruhiwa

Chagueni Viongozi Wanaofaa-Biteko

Elimu Ya Fedha Yafika Makanya Same

COSTECH, CRDB Foundation Yazindua Mikopo Nafuu Kwa Wabunifu

Spika Ahoji Mwongozo Wa Wanaojitolea Kazin

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article UDSM  Kujenga Jengo La Kisasa La Bil 8.3
Next Article Chalamila Atoa Wiki Mbili Wafanyabiashara Ndogo Ndogo Kufungua Njia Kariakoo
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Miaka Minne Ya Samia Na Sekta Ya Elimu
Habari May 28, 2025
Chalamila Atoa Wiki Mbili Wafanyabiashara Ndogo Ndogo Kufungua Njia Kariakoo
Habari May 28, 2025
UDSM  Kujenga Jengo La Kisasa La Bil 8.3
Habari May 27, 2025
Wanazuoni Kujadili   Dira  Itakayojenga  Uchumi Unaofikia   Dola Trilioni Moja
Habari May 26, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?