Na Mwandishi Wetu
RORYA, MARA: MGOMBEA Urais wa NCCR-Mageuzi, Ambar Haji Khamis, amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 29, akisisitiza kuwa ndio njia halali ya kubadilisha uongozi usiofaa.
Akizungumza na wakazi wa Rorya, Khamis amesema wananchi wasikubali kushawishiwa na propaganda zinazolenga kuwazuia kushiriki uchaguzi, kwani kufanya hivyo ni kuikataa haki yao ya kikatiba.
“Ni wajibu wa kila mmoja kutumia kura yake kwa uadilifu ili taifa lipate viongozi wenye maadili, uwajibikaji na uchungu wa kweli kwa maendeleo ya Watanzania,” amesema Khamis.