MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Mbarawa Aitaka Jamii Kulinda Miundombinu ya Uchukuzi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Mbarawa Aitaka Jamii Kulinda Miundombinu ya Uchukuzi
Habari

Mbarawa Aitaka Jamii Kulinda Miundombinu ya Uchukuzi

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: WAZIRI wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, amewataka Watanzania, sekta binafsi na wadau wote kushirikiana na Serikali katika kulinda na kutunza miundombinu ya uchukuzi kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Akizungumza na waandishi wa habari,  kuhusu mafanikio ya Sekta ya Uchukuzi ndani ya siku 100 za Serikali ya Awamu ya Sita, Kipindi cha Pili chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Profesa Mbarawa amesema mafanikio hayo ni ushahidi wa dhamira ya Serikali kujenga miundombinu ya kisasa, salama na yenye tija kwa maendeleo endelevu.
Habari Picha 11043
Amesema katika kipindi hicho, Serikali imepiga hatua kubwa katika kufufua Reli ya Tanzania na Zambia  (TAZARA) ikiwemo kukamilisha majadiliano na kusaini mkataba wa uboreshaji wake Septemba 29, 2025 kati ya Tanzania, Zambia na Kampuni ya China ya Ujenzi wa Uhandisi wa Kiraia (CCECC).
Ameongeza kuwa, utekelezaji wa mradi unatarajiwa kuanza Juni mwaka huu 2026 na utaongeza ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam, biashara ya kikanda na ajira.
Kwa upande wa reli, Serikali imekamilisha upembuzi yakinifu wa reli za kisasa Dar es Salaam na Dodoma, kuimarisha uendeshaji wa reli ya kisasa ya SGR na reli ya zamani ya MGR, kuongeza vitendea kazi vya usafirishaji wa mizigo, pamoja na kuendelea na ujenzi wa reli ya SGR awamu ya kwanza na ya pili.
Aidha, Shirika la Reli (TRC) limeanza kujitegemea kifedha na kuanzisha kampuni tanzu ya Kampuni ya Reli Tanzania (TANRAIL) kuongeza mapato.
Katika sekta ya bandari na usafiri majini, Serikali inaendelea na upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam, maandalizi ya Bandari ya Bagamoyo, ujenzi wa bandari na meli katika Maziwa Makuu pamoja na kuboresha usalama wa majini kupitia vituo vya uokoaji na boti za kisasa.
Serikali pia imeendelea kuboresha viwanja vya ndege, kupanua huduma za ATCL na kuimarisha uunganishaji wa kikanda na kimataifa, hatua inayoiweka Tanzania kama kitovu cha biashara na usafirishaji Afrika Mashariki na Kati.

You Might Also Like

Mfumo Wa KieletronikiWa Albino Kurahisisha Kuwatambua – Ridhiwani

TARURA Yatoa Elimu Nane Nane

Jeshi La Polisi Kufanya Ukaguzi Wa Hali Ya Juu Kwa Mashabiki Katika Mechi Za Simba Na Yanga

BRELA Yazindua Baraza La Wafanyakazi

Tanzania Yapongeza China Kwa Kuimarisha Uhusiano Wa Kidiplomasia Kupitia Lugha, Utamaduni

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Serikali Kuwasilisha Bungeni Nyenzo Kuu Tatu Zitakazowezesha Utekelezaji Dira 2050
Next Article Serikali Yaendelea Kuimarisha Uhuru wa Mahakama – Nchimbi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mbunge Asisitiza Sheria za Majiko Safi Ili Kulinda Mazingira
Habari February 3, 2026
Mwalunenge: Bila Rasilimali Watu Na Mtaji, Mipango Ya Kilimo Haitafanikiwa
Habari February 3, 2026
Gulamali Ahoji Bungeni Changamoto ya Mawasiliano Ilongelo
Makala February 3, 2026
Serikali Yaendelea Kuimarisha Uhuru wa Mahakama – Nchimbi
Habari February 2, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?