Aahidi kuwakomboa wanawake
Na Mwandishi Wetu
KIPENGA cha uchaguzi kimelia na hivi sasa watu wamejitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.
Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Katavi Martha Festo Mariki ni miongoni mwa watia nia katika nafasi hiyo ya ubunge wa Viti maalumu kupitia chama cha Mapinduzi(CCM).
Akizungumza Julai 30, 2025 jijini Dodoma, Martha anasema anawania nafasi hiyo kwa awamu nyingine ili aweze kuwapigania wanawake kuhakikisha wanaondokana na changamoto ya uzazi ili kupunguza vifo vitokanavyo na kadhia hiyo.

Martha ambaye amekuwa mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Katavi anataka kutetea kiti hicho kwa awamu nyingine kwa nia na dhamira ya kuhakikisha vifo hivyo vinapungua kwa kiasi kikubwa katika mkoa wake.
“Niliingia ubunge mwaka 2020 nikilenga kuhakikisha napambana kuhakikisha nashughulika na kero na changamoto za mkoa wangu wa Katavi
“Kabla ya kuwa mbunge nilikuwa mwanachama wa CCM na niligombea kupitia nafasi za wanawake mikoa na nikafanikiwa kuingia na kwa mara nyingine naomba ridhaa tena.
“Kwa ujumla nawashukuru wana CCM Katavi kwa namna ambavyo wanawaamini vijana na wakanipatia nafasi hii lakini serikali yetu pia inavyoamini vijana
“Ninawashukuru kina mama wa Katavi kwa imani yao waliyonipa kwa kuniamini nikawawakilisha kama mbunge kijana,”anasema Martha.
Anaeleza kwamba katika kipindi hiki cha awamu nyingine nawaomba waendelee kuniamini kwani bado nina nia na sababu ya kuendelea kuwatumikia na wananchi wote Kwa maendeleo endelevu ya Katavi na taifa kwa ujumla.
Anaweka wazi kwamba ndoto yake kwa wanawake wa Katavi ni kupunguza changamoto zote hasa za uzazi
“Katika hili tunamshukuru rais Samia Suluhu ambaye ni rais wa kwanza mwanamke na kwa kiasi kikubwa amejikita kutatua changamoto zinazowakabili wanawake nami naungana naye kuhakikisha tunaendelea kutatua changamoto za wanawake nchini hasa katika mkoa wangu wa Katavi,” anasema.
Anapongeza pia serikali kuendelea kupunguza vifo vya watoto wadogo wenye umri chini ya miaka mitano kwa na kuboresha mazingira mazuri kwa kina mama wanaojifungua
“Ikiwa nitapata tena ridhaa ya kukalia kiti hiki nitafanya makubwa zaidi ya awamu iliyopita kwa kuhakikisha nawainua wanawake katika miradi yao wanayoianzisha ili wajikwamue kiuchumi,” anasema Martha.
Nitahakikisha nasimamia ndoto za vijana kutimia katika kuhakikisha nakuwa karibu nao hatua kwa hatua kwa ari na mali kwani vijana wengi hivi sasa wamekuwa wakishindwa kufikia malengo yao kutokana na kukumbwa na vishawishi ving