Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri wa Ardhini (LATRA), itatoa adhabu kwa wale ambao hawajakamilisha utaratibu huduma wa mifumo za mauzo ya tiketi kwa njia ya mtandao.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa LATRA, Salum Pazi amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mchakato huo katika Viwanja vya Maonesho ya Sabasaba kwa mwaka huu 2025.
Pazi amesema, “Ninawakumbusha watoa huduma wa mifumo ya mauzo ya tiketi kwa njia ya mtandao kwamba leo Juni 30, 2025 ndio siku ya mwisho ya kukamilisha taratibu zetu.
“Kwa hiyo wataalamu wanaendelea kufanya uchambuzi wa hiyo mifumo na kufikia Julai Mosi, 2025 mamlaka itatoa hali ya nini kinaendeleakwa wale ambao hawajakamilisha huo utaratibu,” amesema.
Amesisitiza kuanzia Julai mosi 2025 hawataruhusiwa kutoa huduma.
Amesema msmlaka hiyo itaonesha nani amekamilisha tayari, nani bado na uamuzi wa serikali utakaochukuliwa.